kwamamaza 7

Rayon Sports yaondoa ngazi zake zote za uongozi na kuweka kamati ya muda

0

Hatua hii imefuatia kutoelewana kati ya viongozi wa timu hii kulikofanya  kuchukua uamuzi wa kutofautiana kati yao na kufanya timu kutokuwa na msimamo thabiti.

Uamuzi wa kuondoa ngazi za uongozi za  Rayon Sports umechukulina na kundi la washauri na wafadhili wa Rayon Sports linalojulikana kama “Imena” katika kikao kilichofanyika siku ya jana kwenye Hoteli ya Serena.

Ngazi zilizokuwa na uadhifa wa kuingoza Rayon Sports ni pamoja na Bodi ya timu ambayo imekuwa ikiongozwa na (Bw Charles Ngarambe), Kamati ya Shirika la Rayon Sports ambayo imekuwa ikiongozwa na (Bw Kimenyi Vedaste) halafu na Kamati kuu ya Rayon Sports ambayo kiongozi wake amekuwa(Gacinya Denis).

Mkutano huu ulikuwa umewaleta pamoja watu wenye hadhi mbalimbali kwenye timu ya Rayon Sports wakiwemo waliokuwa viongozi wa Rayon Sport na mashabiki wake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Uamuzi wa mkutano huo ulikuwa kuondosha kamati hizi zote na kuweka kamati ya muda ambayo itashughulikia na mambo muhimu yanayohusu uongozi wa Rayon Sports na hata kuandaa uchaguzi wa kamati zitakazoiongoza timu hii.

 

Kamati iliyowekwa inaundwa na Ngarambe Charles, Gacinya Denis na hata Rudasingwa Theogene ambao watakuwa wakishika kiti cha kuongoza timu hii mpaka uchaguzi wa viongozi rasmi kufanyika.

Uamuzi wa kuondoa uongozi wa timu ya Rayon Sport unachukuliwa kufuatia habari zilizoenea katika vyombo vya habari kwamba Olivier Karekezi ameteuliwa na timu ya Rayon Sports kuwa kocha mkuu na baada ya muda si mlefu mojawapo wa viongozi wa Rayon Sports wakakanusha habari hizi kwa kusema ni uamuzi usiokuwa wa pamoja. Uamuzi uliofuata ni wa kuacha nafasi hiyo ya kocha kupiganiwa upya.

Ni mara nyingi kuliposikika matatizo baina ya viongozi wa timu ya Rayon Sports kitu ambacho huwakera washabiki wa timu hii iliyoingia nyoyo za wengi hapa nchini na nje.

Uamuzi wa kuondoa viongozi wale ulitangazwa kwenye barua iliyoandikiwa vyombo vya habari.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.