kwamamaza 7

Rayon Sports yamteua aliyekuwa nahodha wa timu ya Rwanda kama meneja wake mkuu

0

Baada ya pande mbili kufikia makubaliano juu ya mkataba wa miaka miwili Olivier Karekezi atatangazwa mnamo siku chache zijazo kama kocha mkuu wa Rayon Sports.

Alipoongea na gazeti la New Times la Rwanda Gacinya ambaye ni Kiongozi mkuu wa Rayon Sports amekiri kwamba wamekwisha fikia makubaliano ya mkataba utakaomfanya kushika uadhifa wa umeneja wa timu hiyo hadi msimu wa 2018/2019.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“ni ukweli tumekwisha kubaliana na Olivier Karekezi juu ya mkataba wa miaka miwili ya kuifunza Rayon Sports lakini niweke wazi itategemea na matokeo ya kazi yake mkataba unaweza ukasitishwa awali ama hatua ya kuendelea na kazi yake kuchukuliwa ikiwa takuwa akifanya vizuri.

Olivier Karekezi atakuwa na makocha wasaidizi wawili ambao pia walicheza pamoja kwenye timu ya Taifa Amavubi miaka michache iliyopita. Makocha hao ni Ndikumana Hamad Katauti aliyekuwa akifanya kazi kama kocha msaidizi wa timu ya Musanze FC msimu uliyopita  na hata Nkunzingoma Ramadhan.

Kocha huyu mpya wa mabingwa wa Rwanda yuko bado,Sweden ambako amekuwa akifunza timu ya vijana chini wa miaka 17, na ana Cheti cha Kufundisha cha shirikisho la UEFA cha kiwango A.

Karekezi pia ambaye ana umri wa miaka 34, ametunukiwa zawadi ya Kocha mzuri wa vijana mwaka jana.

Kocha huyu ambaye anatarajiwa kutua Rwanda kupiga saini ya mkataba na Rayon Sports atakuwa akifanya kazi kwa mara ya kwanza kama kocha mkuu. Karekezi anatarajiwa kuingoza timu ya Rayon Sports kutetea taji lake na hata kujaribu kufanya vizuri kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.