HABARI MPYA

Rais Paul Kagame ahudhuria kuapishwa kwa Rais wa Angola

Rais Paul kagame amehudhuria sherehe ya kula kiapo ya mwenzake wa Angola,Joao Lourenco.

Rais Kagame akihojiana na mwenzake wa Angola,Joao Lourenco

Rais Kagame amefika nchini Angola jana kama inavyonekana kwenye Twitter ya ikulu ya Rwanda.

Kunatarajiwa kuwa Rais aliyechaguliwa nchini Angola,Lourenco Joao atakula kiap oleo tarehe 26 Septemba 2017.

Joao Lourenco alishinda uchaguzi wa rais tarehe 24 Agosti 2017 kwa kura 64.5%, ni mwanachama wa MPLA baada ya Edouardo Dos Santos kutangaza kwa nia kwamba hatawania uchaguzi wa rais.

Angola ni nchi yenye idadi ya watu miliyoni 25 na ya pili barani Afrika kwa kuuza petroli kwani inauza pipa 1680 kila siku.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top