Connect with us

HABARI MPYA

Rais Kagame yatarajiwa kuwa jibu kwa jamhuri ya Afrika ya kati atakapongoza UA

Published

on

Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajiwa kutoa msaada mkubwa wa kutatua changamoto kadhaa za jamhuri ya Africa ya kati atakapoanza uongozi wake wa Umoja wa Afrika tarehe mosi Januari 2018

Rais Kagame akimusalimu  Rais Archange Touadera

Kupitia taarifa ya mondeafrique.com inaonyesha kuwa rais Kagame anaipa bara la Afrika na wanafrika nafasi ya kwanza na kuwa  anahamasisha wanafrika kwamba hawana budi kujitatulia changamoto zao kabla ya msaada kutoka ugenini na kuwa siyo lazima kufuata demokrasia ya Wazungu kinyume na mahitaji ya bara la Afrika.

Pengine,habari yenye kichwa “Centrafrique,le Rwanda a la manoevre” inaeleza kuwa Rais Kagame alionyesha namna ambavyo Ufaransa na Umoja wa Mataifa wameshindwa kutatua changamoto zilizoko nchini jamhuri ya Afrika kati na kwa hiyo Rais Kagame   anatarajiwa  kutoa msaada kamili kwa mwenzake,Touadera ili kusuluhisha matatizo kadhaa ya nchi yake.

Haya ni maoni yanayosisitizwa na barozi wa Ubelgiji kwa Rwanda kuwa Rais Kagame ni kama mwalimu mkuu (patron) wa Afrika kulingana na namna anavyongoza baada ya ushindi wa uchaguzi tarehe 4 Agosti 2017 kwa 98.79% na kula kiapo kwa shangwe,nderemo na hoihoi katika sherehe iliyohudhuliwa na marais na wakuu wa serikali 19.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *