kwamamaza 7

Rais Kagame azifikia wilaya tatu Nyamagabe, Huye na Kamonyi siku moja akiwa kampeni

0

Mh. Rais Paul Kagame ambaye ni mgombea wa kiti cha Urais kwa tiketi ya chama chake cha RPF ameendelea na ziara yake kwa siku ya tatu wakati huu akizuunguka wilaya tatu ambazo ni Nyamagabe, Huye na Kamonyi.

Ziara yake ya kampeni Nyamagabe

Umati wa watu

Mh. Kagame alitua Nyamagabe mnamo saa nne za asubuhi ambapo amewakuta raia chungu nzima waliokuja kumpokea na kumwonyesha kuwa wanamwunga mkono kwenye uchaguzi ambao unafanyika hapo mwezi Agosti.

Raia hao ambao wamekuwa wengi kweli kweli walipomwona walishangilia sana huku akizuunguka umati kwa kuwasalimu. Wanakiri kwamba waliamka saa tisa za asubuhi wakija kumpokea mgombea wao.

Mwanachama wa RPF katika wilaya hiyo ambaye pia ni mratibu wa kampeni za mgombea wa chama cha RPF amesema kwamba wanajivunia kuwa hawaitwi kamwe jina la Abatebo na wanaitwa badala yake aba “Tres Bon”.

Katika hafla hiyo kulikuwa na wafuasi wa vyama vingine vilivyotangaza kwamba vitamwunga mkono rais mgombea wa RPF ambaye ni Paul Kagame.

wafuasi wa chama kingine

Kagame alipohutubia alianza kwa kuwashukuru raia hao kwa kuwa wamekuja kumwunga mkono

Aliwakumbusha kwamba maisha ya moja wao yalibadilika bora mno na kuwakumbusha kwamba wale ambao hayajabadilika ni ziara inayoendelea na ambayo itaanza tarehe tano Agosti.

Aligusia kuhusu jina la utani ambalo raia wa Nyamagabe walikuwa wakiitwa la “Abatebo” na kulihusisha na msemo wa Kinyarwanda unaosema “mwenye kujifanya tonga hukamata jivu” na kusema mambo kwa hivi yamebadilika na watu kwa sasa wanakamata fedha.

Aliendelea kuwaonyesha kwamba kuna mengi yaliyofanywa na ambayo ataendelea kuwekwa nguvu kama Umeme kwa kuusambaza kwa wananchi karibu au wote.

Hakukosa hata kuwaahidi kwamba barabara inayowaunganisha na Huye- Nyamagabe na Rusizi itaengenezwa karibu iwezekanavyo.

 

Alitamatisha shughuli zake hapo kwa kuwakumbusha kwamba tarehe ya kuhakikisha hayo yote yanafikiwa ni tarehe nne Agosti. Na akaendelea na ziara yake kwenye wilaya ya Huye

Paul Kagame akiwa kampeni-HUYE

Kagame akiwa Huye

Kama ilivyokuwa awali alipokuwa kwenye wilaya ya Nyamagabe hapa napo aliukuta umati wa watu wengi waliokuja kumpokea na kumpongeza kwa yale waliyokwisha fikia.

Wakimsubiri raia hao wamekuwa wakiburidishwa na ngoma za wasani mbalimbali ambazo nyingi zilikuwa ni za kumsifu.

Akifika pale aliwapa mifano halisi ya yale aliyoahidi na kwamba yalifikiwa na kusema kwamba mengine zaidi yamo njiani.

Katika maneno yake alisema “tunachagua wengi wazuri badala ya wengi wabaya, kwa desturi ya RPF tunapenda kwenda kwa kushikana mikono”

Amegusia pia kwamba sera na miundombinu kwa ajili ya maendeleo walioahidiwa raia walifanyiwa na kwamba zinaendelea na kuwahimiza vijana kutumia fursa walizo nazo ili kujiendeleza.

Baada ya hapo rais Kagame aliendelea na ziara yake kwenye wilaya ya Kamonyi

Paul Kagame akiwa kampeni Kamonyi

Kama ilivvyokuwa kwenye wilaya nyingine alizitembea rais Kagame hapa napo kulikuwa na umati wa watu wengi sana waliokuwa wakimngoja huku wakiburudika kwa miziki ya wasani mbalimbali

Rais Kagame alipotua hapo kumefuata muda wa kusikia ushahidi wa jinsi wananchi walivyojiendeleza kwa sababu ya utawala wa RPF na hapo ukatolewa na raia anayetambulika kama Mukamusoni Francine.

 

Mgombea wa chama cha RPF Paul Kagame alipohotubia aliwashkuru watu ambao wamekuwa pamoja kwenye ziara yote ya Nyamagabe-Huye na Kamonyi.

Aliendelea kubainisha kwamba kura hiyi itakayofanyika inabeba maana ya historia ambayo Rwanda iliipitia na kusema kwamba safari hii ambayo imedumu kwa miaka 23 ambapo wanyarwanda walikuwa wamezikwa na wakafufuka na kupiga hatua ya maendeleo.

Aliwagusia wale wanaopinga sera za serikali kwamba ni wale wenye kukosa historia ya Rwanda. Hapa amewaonyesha wananchi kwamba ziara inaendelea.

Katika ziara zake, kuhusu sera ya kujiendeleza hakosi kugusia umeme na hapa amesema kwamba ingawa idadi nyingi ilikwishaupata umeme kunahitajika kuusambaza pote.

Kabla ya kuwaomba kumpa kura kwa wingi ili mipango yake ije ikatekelezeka amepata fursa ya kuwaomba vijana kufumbua macho na kuongeza bidii kwa kufanya kazi kwa pamoja licha ya kuwa hawafahamu mengi ya kabla ya miaka 23 iliyopita.

Kwa kukamilisha ziara yake ya siku aliwaomba kumpa kura asilimia 100 kwa sababu anawaamini kuwa wafuasi wa dhati na wanaojua yale wanayotaka kuyafikia.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.