kwamamaza 7

Rais Kagame awaonyesha wanaohudhuria mafunzo siri yake kushinda vita vya ukombozi

0

Imekuwa ni muda wakuwahimiza waliohudhuria mafunzo ya maadili ,mila na tamaduni za wanyarwanda kushikilia mafunzo waliopewa na kuyatumia wakati yanapohitajika kutumiwa hasa kwa kuilinda nchi dhidi ya hadui wake.

Jana tarehe 13, rais Paul Kagame ameongoza hafla ya kukamilisha mafunzo ya ya maadili ,mila na tamaduni za wanyarwanda yaliyopewa wahitimu na wanafunzi wa vyuo waliohitimu kutoka nje ya nchi wanaojulikana kama Indagamirwa katika kikosi chao cha 10 kilichofanyia mafunzo yao Gabiro, kwenye wilaya ya Gatsibo.[xyz-ihs snippet=”google”]

[xyz-ihs snippet=”google”]

Alitumia bunduki ambayo inawatumiwa kupigana vita kuwaonyesha namna ilivyomsaidia wakati wa vita kwa kupigana na kwa kuitumia katika shughuli nyingine kama vifaa na kwa hivyo ni fursa ya kuwahimiza kuiga mfano huo wa majeshi yaliyokuwa ya RPA kwa kujitafutia suluhu kwa matatizo yanayowakumba.

“Kwenye bunduki ya Ak 47 kuna taa la manjano ikiwa ni wakati wa jioni na giza humyasa. Haya, nalotaka kuwaambia ni kuhusu kujitafutia njia, mnaona natumia miwani ili  niweze kutizama vizuri kwa macho, ikiwa ni wakati wa jioni ningemwambia mtu kuenda mbele kwa kuniongoza na nikatumia taa hilo na tukaweza kufika ambapo tunataka kwenda”

Rais Kagame aliendelea kusema kwamba kwa hivi, Rwanda imeyapitia mengi ambayo yamekuwa ni somo kwa upande wake ni hilo litawasaidi kujiendeleza na kuilinda nchi kupitia misingi imara ya wazalendo wake.

Hajaacha kusema pia kuhusu wanaothubutu kuishambulia nchi na kueleza kwamba mwenye makusudi hayo hangekosa kupata somo kwa kuwa wanyarwanda walipitia nyakati ngumu ambazo kwao haziwaruhusu kufanya kosa lolote.

“Yeyote ambaye angethubutu kutuchochea angeona,Huwa tunasikia wale wanaosema waache waseme maneno hayatudhui, hatujui kupambana vita vya maneno na najua maneno yao hayatawaleta popote. Lakini tunachotaka ni kujenga nchi yetu bila yeyote kuvuruga yaani tukiishi kwa usalama…”

Amewafafanulia kuwa “palipo na nia pana njia” kwa kuwa nguvu walizo nazo ndizo zitakazo wawezesha kuyafikia malengo ya nchi inayolenga kuyafikia ikiwa vijana hao watajitolea kuchangia kwa nguvu zao.

Waziri wa Ulinzi Gen. James Kabarebe naye alichukuwa muda wake kuwashukuru vijana hawa waliohudhuria mafunzo haya na kuwaambia kwamba wanayapata katika wakati mwafaka. Alisema kuwa walifunzwa pia namna ya kujipanga katika vita.

Indangamirwa

Mwenyekiti wa Tume ya Itorero ameonyesha kuwa vijana wengi walijisali wakitaka kuhudhuria mafunzo haya ila wakati haukuwaruhusu kwa kuwa kulikuwa na mabadiliko ya hapa na pale kwa ratiba yake na hivyo kufanya mafunzo haya kugongana na shughuli zao muhimu.

Vijana hawa waliohudhuria mafunzo wanaojumuika katika kikosi cha ‘Indangamirwa’ walikuwa 523 ambao ni mojawapo wa jumla ya vikosi 9 ya  waliohudhuria mafunzo ya Gabiro. Kwa mwisho wa mafunzo haya takriban vijana 137 walijisajiri kujiunga na jeshi kwa nia yao ambapo watapitia kwenye chuo cha Kijeshi kupata mafunzo ya ziada.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.