kwamamaza 7

Rais Kagame atua Israel kwa ziara ya kidiplomasia

0

Inasemekana kuwa rais Paul Kagame amewasili nchini Israel katika ziara ya siku mbiri ambayo ina madhumuni ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.

Rais Kagame anatua nchini Israel kwa mara ya kwanza tangu 2008 alipokuwa akijiunga na nchi katika sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya kufahamika kama nchi huru baada ya maafa ya mauaji ya kimbari dhidi ya wayahudi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hata hivyo Ikulu ya Rwanda haijathibitisha habari hizi kwa mujibu wa habari iliyotangazwa na i24News gazeti la habari la Israel.

Nchi hizi mbili zimekuwa zikionyesha kuujenga uhusiano imara wa kidiplomasia ikihusishwa pakubwa  na historia sambamba za mauaji ya kimbari yaliyozikabili nchi hizo mbili.

Zaidi ya hayo nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana katika Nyanja mbalimbali zikiwemo kijeshi kwa majeshi ya waisrael wakiwapa mafunzo ya kijeshi na hata katika elimu ambapo wanafunzi wa Rwanda wakisafiri kwa ajili ya masomo nchini Israel.

Rais wa Rwanda pengine aligusia mambo haya mwaka jana alipokuwa Marekani wakijadili uhusiano wa Marekani na Israel  na kuonyesha kwamba haungi mkono azimio la UN lililokuwa linatarajiwa kuidhinishwa kuhusu kubadili mpaka ya Israel kwa maslahi ya Palestine.

Ziara hii ya Rais Kagame inajiri baada ya ile ya mwaka jana ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Nyetanyahu kuizuru Rwanda na kuisifu kwa hatua ya kimaendeleo ambayo nchi hii inazidi kupiga.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.