BIASHARA

Rais Kagame ataka serikali za Afrika kuanzisha mazingira bora ya kiuchumi

Rais Paul Kagame kwenye mkutano wa kiuchumi mjini Sharm el Sheikh nchini  Misri, ametaka serikali za Afrika kutoa mazingira bora ya shughuli za uchumi.

Rais Kagame amekumbusha kuwa maendelo ya kuchumi barani yatapatikana kupitia sekta binafsi na kwa hiyo haina budi kuboresha mazingira ya kiuchumi.

Rais Kagame amesema”maendeleo ya uchumi wa Afrika yatawezekana,ila kunahitajika kukuza sekta binafsi.Hata hivyo,serikali inapaswa kuboresha mazingira ya shughuli”.

Rais Kagame ameongeza kuwa bara la Afrika linahitaji kuharakisha na kutopoteza fursa.

Mkutano huu umehudhuriwa na wakuu wa serikali pamoja na wekezaji mbalimbali kutoka pande zote za dunia.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top