Connect with us

HABARI MPYA

Rais Kagame ampongeza Kenyatta kwa kushinda uchaguzi

Published

on

Rais wa jamhuri Paul Kagame amemtumia pongezi mwenzake rais mteure wa kenya ambaye ameshinda kuongoza muhula wake wa pili.

Akitumia mtandao wake wa twitter, rais Kagame, amempongeza akisema: “nakutakia kila la heri ndugu Kenyatta kwa ushindi mkubwa na upendo wa wakenya kwako.”

Aendelea akisisitiza kuwa umoja na ushirikiano uliyopo kati ya nchi hizo mbili, ni lazima kuimarishwa na hasa hasa ni nchi za jumuiya ya Afrika ya mashariki(EAC).

Wakenya waliamua mnamo tarehe 8 mwezi wa 8 ambapo Uhuru Kenyatta amepata ushindi wa asilimia 54.7 ya kura kwa mpinzani wake Raila Omoro odinga, ambaye hakuridhika na matokeo, amepata asilimia 44.7.

Uchaguzi huu wa Kenya umefanyika mara baada ya uchaguzi wa Rwanda ambao ulinyakuliwa na mgombea wa chama cha RPF na kishindo kikubwa cha asilimia 98.79 ya kula. Raisi Kagame kama mwenzie wa Kenya amepongezwa na marais wenzake, akiwemo Kenyatta, wakati aliposhinda uchaguzi kwa muhula ambao utatimizwa mnamo mwaka 2024.

Viongozi kadhaa ulimwenguni huenda wakamtumia pongezi, Kenyatta, wakimtakia kila la kheri kwa miaka mitano zaidi madarakani akiwa anawaongoza wakenya. Mmojawao wa hao viongozi ni raisi wa Burundi Nkurunziza ambaye alimtumia pongezi wakati wa matokeo ya muda. Uchaguzi wa Kenya ulikuwa na wagombea 8.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *