kwamamaza 7

Rais Kagame afunguka atakavyoondoka madarakani

0

Rais Kagame wa Rwanda ameweka wazi atakayeshika mikoba yake kwa nafasi ya Urais.

Kwa mujibu wa Gazeti la Time Magazine nchini Marekani, Kagame alisema kwamba urais utashikwa na mtu mwingine ambaye si mwanachama wa chama tawala, RPF-Inkotanyi.

Amesema kinyume na hili, ni kujenga ufalme ama kitu kingine sawa.

Kwa kujibu kama chama chake kinamuandaa mgombea atakayeshika mikoba yake, Kagame alisema:

“  Ikiwa hivyo, ni kama ufalme au vingine sawa ni hilo.” Alisema

Akizungumza kama aliomba mhula wa tatu kinyume na katiba la nchi, Kagame alisema kwamba yeye alikuwa anataka kuondoka madarakani lakini hakuweza kutokana na maombi ya wananchi.

“ Mimi nilitaka kuondoka. Nilileleza hata sababu lakini wengi waliamka na kuniomba, tupatie muda mwingine, tupatie fursa nyingine(…).”

“ Kulikuwepo maoni mengi lakini nami nikakubali.” Aliongeza

Rais Kagame anaongoza Rwanda tangu mwaka 2003.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.