kwamamaza 7

Rais Kagame afafanua maana ya siku ya Ukombozi katika maadhimisho yake.

0

Ikiwa leo ni tarehe 04 Julai 2017 ambapo Rwanda inaadhimisha siku ya Ukombozi kwa mara ya 23 ampapo sherehe za kuadhimisha siku hiyi zimefanyika katika wilaya ya Nyabihu ambako rais Kagame amejiunga na raia wa hapo kuadhimisha siku hiyi na imeendeshwa pamoja na sherehe za kuzindua majengo mbalimbali ya miundobinu.

Rais Kagame akiwa pamoja na mkewe Bi Janet Kagame, alihotubia mbele ya maelfu ya raia wa wilaya zinazopakana na tarafa ya Shyira ambazo ni Gakenke, Musanze na Muhanga , Ngororero na hata wa Nyabihu ambako tarafa hiyo iliyopo.

Katika hotuba yake ,rais Kagame aliwaelezea raia hao nini maana halisi ya kujikomboa isiyo ile maana ya juu. Alianza kwa kuwatakia Wanyarwanda siku kuu ya kujikomboa kwa mara ya 23 na kuongeza kwamba wengi wa Wanyarwanda hawakuwa wajazaliwa.

Akieleza nini maana ya kujikomboa alisema inajumuisha maana mbili

“tumeondosha utawala mbaya ambao ungetufanya kufuata mkia kulingana na watu wa nchi nyingine”.

Aliendelea kusema kwamba kujikomboa kunajumuisha kufukuza  utawala mbaya  na athari zake zikiwemo njaa, umaskini na hata migogoro.

“Tumewahi kuondosha utawala mbaya. Tunalolikabili sasa ni athari za utawala mbaya. Tunahitaji kila yeyote kujikomboa na tuna imani itakuwa rahisi kwa kuwa tumekwisha ona kwamba inawezekana”

[xyz-ihs snippet=”google”]

Rais aliwakumbusha pia Wanyarwanda kwamba siku ya Ukombozi ni siku ya kufikilia kuhusu yale pale ambayo nchi imetoka na pale inapoelekea.  “tunataka kujiendeleza tukiwana misingi imara ya Uchumi ambayo tunahitaji. Yale ambayo tunawafanyia wanyarwanda ni chanzo cha njia ya kujijenga”.

Siku hii ambayo inaadhimishwa leo tarehe 04 inajumuishwa na siku ya Uhuru ambayo inaadhimishwa tarehe 1 Julai ambako Rwanda ilipata uhuru tarehe sawa mwaka 1962.

Sherehe hiyo ilifanyika moja kwa moja na shughuli za kuzindua Hospitali ya Shyira iliyokwisha jengwa hivi karibuni na kulizinduliwa pia makaazi ya pamoja ambayo atawahudumia familia 108 zisizojiweza.

Wanyarwanda waliamua kusherehekea Uhuru pamoja na siku ya Ukombozi ambayo kulingana na wanasiasa pamoja na raia wengine ndio wanaona yenye maana zaidi kwa kuwa kunakumbukwa wakati ambapo waliokuwa majeshi wa APR walikatisha mauaji ya Kimabari dhidi ya Watutsi ya 1994.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.