kwamamaza 7

Polisi imeamuru wandugu wawili kubadili wake wao

0

Waume wawili wa sehemu ijulikanayo kwa jina la Butende-Bubanda, wilaya ya Kamuli nchini Uganda, wamekubaliana kubali wake wao ili waweze kutatua swala lililo dumu siku nyingi.

Paul Kiirya, mwenye umri wa miaka 55 na Kagoda Malinzi mwenye umri wa miaka 40 walifanya muda murefu katika magomvi kwa ajili ya wanawake.

Mwanzo Kiirya alienda kwenye stesheni ya polisi kushitaki nduguye mdogo Malinzi akimushutumu kumunyanganya mke wake waliozaa watoto 11 pamoja.

Eti “nataka mke wangu aje tuishi pamoja, tumefanya miaka 32 tukiishi pamoja, tumezaa watoto 11, sipendi kumupoteza”.

Dennis Mudyope, kiongozi wa polisi katika wilaya hio anahakikisha ya kuwa Kiirya ndie alianza kuchukuwa mke wa nduguye mdogo mwaka wa 2016.

Wakati huo Malinzi alikuwa amefukuza mke Proscovia Namugaya mwenye umri wa miaka 35, kiisha Kiirya akamupokea na kukodi chumba kwa ajili yake na kumufanya mke wa inne.

Malinzi alipo jua ya kwamba mkubwa wake amechukua mke wake alijaribu kumurejesha ikawa bure na ndipo Malinzi akaanza kutongoza mke wa mkubwa wake Katirini Nabirye, Kiirya na mwisho akauepa moyo wake hadi kumuchukuwa kwake, wakati Kiirya alipogundua hayo akahuzunika moyoni na kwenda kumushitaki kwenye stesheni ya polisi kama vile husema The New Vision.

Nabirye alikataa kurudi kwa mumeo Kiirya akisema amejibiwa kwa kuwa aliteswa muda wa miaka 12, ila anasema ya kuwa ombi lake limejibiwa, anasema ya kuwa Kiirya alikuwa akitongoza wake wengine na kukodi nyumba kwa ajili yao.

Kiirya yeye husema ya kuwa mdogo wake amemutia kidonda ambacho hatasahau hata siku moja eti “Malinzi aliishi kwangu nyumbani akiwa mtoto, mke wangu alikuwa akimunawisha, hasa ni vipi yawezekana awe mke wake? Sherti arudishe watoto wangu”.

Baada ya kuona hakuna mke anaye hitaji kurudi kwa mumeo, polisi iliamua ya kuwa hao wandugu kubadili wake kwa kuwa hata watoto wao wana uhusiano wa karibu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.