HABARI

Nyanza:Kijana wa miaka 21 atuhumiwa kuua bibi yake wa miaka 68

Kijana wa miaka 21 kwa jina la Arsene Irakoze anatuhumiwa  kumuua bibi yake,Bernadette Murekatete  ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kiniga,tarafa ya Muyira kusini mwa nchi.

Katibu mtendaji wa tarafa ya Muyira,Valens Murenzi ametangaza kuwa kijana huyu anatuhumiwa kuua bibi yake kwa ajili ya fedha.

Kiongozi huyu ameongeza kuwa Arsene ameiba ng’ombe wa bibi wake baada ya uhalifu huu na kumuuza frw 240,000 kisha akatoweka.

Malehemu alimrea Arsene akiwa mtoto wa miezi miwili baada ya kifo cha mama yake aliyekuwa bintiye.

Polisi inatafuta anapoelekea ili afikishwa mahakamani.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top