Wafuasi wa muimbaji Ngabo Medaly maafuku kama Meddy wamekosoa kwa washiriki wa shindano la Nyampinga 2018 baada ya Meddy kupost hawa warembo wakirudia wimbo wake uliotia fora kwa jina la ‘Slowly’.
Mmoja wao kwa jina la Knightnews250 ameandika kuwa ameshangazwa na namna ambavyo hawa wasichana wanaweza kukumbuka na kuzingatia kila mshororo wa wimbo huu lakini wakashindwa kusoma miradi yaho husika na shindano hili.
Knightnews250 ameandika”Sielewi namna ambavyo wanarudia mishororo yote ya wimbo huu lakini wakashindwa kusoma vilivyo miradi yao kwenye fainali ya shindano”.
Mwingine kwa jina la Chrissbrisspaccy ameandika kuwa anaona kwamba huu ni muda wa kuponda raha kwa hawa wasichana.
Pamoja na hili,wengi mwa Wanyarwanda hasa mitandao ya kijamii hivi karibuni walikosoa tabia za hawa wasichana walipoonekana wakikama maziwa kwa kutumia ndoo za unga ya kufulia.Inaaminika kwamba mhenga na mrembo miongoni hawa ndiye atakayekuwa ‘miss’ wa Rwanda mwaka wa 2018.
Picha ya mmoja mwa hawa wasichana iliyozusha mawazo mengi kwenye mitandao ya kijamii