HABARI

Nyamasheke:Mtoto wa miaka sita afariki kwa kuchomwa na umeme

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka sita kwa jina la Bellange Bimenyimana amekufa baada ya kuchomwa na umeme akiwa chumbani mwake, kijijini Cyivugiza,tarafa ya Kanjongo.

Taarifa hizi zimethibitishwa na katibu mtendaji wa tarafa,Zacharie Twagirayezu kwa kueleza kuwa mtoto huyu jana alipotoka shuleni jioni alingia chumbani mwake ili avue nguo kisha mtumishi wa nyumbani akasikia mlipuko na mtoto akipiga mayowe na kumkuta mtoto amechomwa na umeme.

Kiongozi wa kituo cha umeme katika wilaya,Erneste Hagenimana ameleza kwamba chanzo cha kisa hiki ni ufungaji mbaya wa nyaya za umeme za chumba cha malehemu.

Kiongozi huyu amehamasisha wakazi kutafuta wafundi bingwa wa kufunga vifaa vya umeme katika nyumba zao ili kujilinda ajari.

Malehemu Bimenyimana alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi kidato cha kwanza,kunatarajiwa kwamba atazikwa leo tarehe 23 Septemba 2017.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top