kwamamaza 7

Nyamasheke :Nitawaletea mashua na barabara ya rami- Maahidi ya Dkt Frank

0

Mgombea kwa tiketi ya chama cha Green Dkt. Frank Habineza amekuwa katika wilaya ya Nyamasheke kwa siku yake ya ziara za Kampeni baada ya kutoka kwenye wilaya ya Rusizi hapo tarehe 14 ya mwanzo rasmi ya kampeni.

Dkt.Frank Habineza aliyekuwa pamoja na mke wake akifuatiwa na wanachama wake wa Green, aliwafafanulia, raia wa Nyamasheke ambao hawakuhudhuria kwa kiasi kikubwa, mengi yaliyomo katika mipango yake ikiwemo kuwaletea mashua na barabara ya rami wakazi wa wilaya ya Nyamasheke.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Shughuli hiyo ambayo ilifanyika kwenye tarafa ya Kanjongo kwenye kiwanja cha Kirambo ambako hakuwa na raia wengi waliokuja kusikia kuhusu mengi yaliyomo kwenye mipango ya mgombea huyu ambayo licha ya kuwa atawaletea mashua na barabara ya rami kutoka Kirambo- Tyazo-Rangiro amesema kwamba atayiletea nchi mabadiliko mengi ambayo ataiwezesha kujiendeleza.

Baada ya kukaribishwa na Meya wa wilaya ya Nyamasheke, aliendelea kuzieleza sera zake kwa raia hao badala ya yale aliyoahidi kwamba atawatendea kama maalum, miongoni mwa mengine  aliyowaahidi raia hao ni pamoja na kuwalindia usalama akitumia mifumo ya kimaendeleo ya kuwaletea ndege zisizo na madereva zitakazorahisisha askari wa usalama kutekeleza wajibu wao wa kuulinda usalama.

Sera hiyo ilidokezwa pia alipokuwa kwenye wilaya ya Rusizi na ni sera ambayo ni muhimu kwenye jumla ya mipango yake.

Frank akiwasalimu wananchi

Amesema kuwa atazifanya sera za sekta ya kilimo imara na zenye kueleweka kulingana na zile zilizoko, lingine ni kuuboresha ushirikiano na nchi nyingine za kigeni kama Burundi na hata Ufaransa hapa amewaonyesha kwamba anasikitishwa na jinsi uhusiano wa Rwanda na Ufaransa unavyozidi kudorora.

Hakukosa kudokeza kuhusu magereza yanayowafunga watu kinyume na sheria na hapa kudokeza kwamba ataondosha magereza haya na kuhakikisha kwamba inafanyika kwa mjibu wa sheria. Jambo jingine alilobainisha ni kufutwa kwa kodi ya mashamba.

 

Kwa kutamatisha amesema ana imani kwamba atachaguliwa na kuyatekeleza yote na kuongeza kwamba ingawa hapati wafuasi wengi wakati anapokuwa kwenye kampeni, ana uhakika kuna wanaomwunga mkono ambao watampa kura zitakazomwezesha kushika kiti cha urais.

Mpaka sasa Mgombea huyu amekwisha fikia wilaya mbili ambazo ni Nyamasheke na Rusizi na anatarajiwa kuendelea kwenye wilaya nyingine akieleza sera zake kwa ajili ya  kuwatafuta wafuasi watakaompa kura katika uchaguzi wa mwezi Agosti.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.