Connect with us

HABARI

Nyamagabe: Mwanafunzi afarikia shimoni la maji

Published

on

Mwanafunzi ambaye alikuwa akishiriki na mtihani wa taifa katika shule la Notre dame de la Paix wilayani Nyamagabe, afariki duniani baada ya kutoroka uongozi wa shule na kuenda kuogelea katika shimo la maji na wenzake.

Gasiga Desire mwenye umri wa miaka 19, alikuwa bado kumaliza mtihani wa taifa wa kufunga shule za sekondali; alifariki jana 13 Novemba 216 wakati alipokuwa anaogelea na wenzake tisa ambao walishindwa kumwokoa.

Kiongozi wa kata ya Cyanika-Ndorimana Chrysostome, ambapo shimo hilo la maji lilikuwepo; alithibitisha habari.

“Ndiyo ni ukweli, wanafunzi 10 walitoroka shule na kuelekea kwenye shimo la maji la mahali wachina walipata madini.” Kiongozi alieleza.

Habari ya kifo chake ilijurikana baada ya muda wa saa kupotelea kwa Desire. Uongozi ulijulisha polisi ndipo waligundua maiti yake na raia walihusika na maombolezo wakisubiri shirika za polisi kuikuta maiti.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

@Bwiza.com

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *