HABARI

Nyabihu:Wakazi wanung’unika juu ya uharibu wa mazao yao

Wakazi wa wilaya ya tarafa za Jenda,Karago na Rambura,magharibi kaskazini mwa nchi wametangaza kutofurahia waliliofanyiwa juu mradi wa ujenzi wa umeme utakaotoka nchini Rwanda hadi nchini Ethiopia.

Baadhi ya wakazi hawa wametangazia VOA kuwa wafanyakazi wa mradi huu waliharibu mazao yao kama vile viazi vitamu,miti na maharagwe na kuwa wamemaliza miaka miwili wakisubiri fidia ya mazao yao ila wamekosa.

Hawa wameleza kuwa hasara hii iliathiri mno hali ya maisha ya familia zao kwa kuwa walikuwa wakitegemea sana mazao yaliyoharibiwa kwa kuwatunza wanafamilia wao.

Msemaji wa ofisi kuu ya nguvu,Prosper Mubera ameleza kuwa wengi mwa wakazi hawa walipata fedha zao na kuwa wanaobaki watapata fedha zao hivi karibu.

Huyu amekanusha kwamba hakuna watu waliomaliza miaka miwili bila kupata fedha za fidia ya mazao yao.

Pamoja na haya,mala nyingi wakazi hulalamikia fidia ya mazao yao yaliyoharibika juu ya vitendo vya manufaa ya umma.Sheria ya mwaka 2015 husika na jambo hili,makala yake ya 36 inasema kuwa wakazi wanapata fidia ya mazao yao kabla ya siku 120 za uamuzi wa mradi huu kuanzishwa.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top