HABARI

Nyabihu:Mkazi wa kijiji cha Gaseke ajiua

Mwanamume mkazi  wa kijiji cha Gaseke,tarafa ya Rugera,Anastase Nturanyenabo,67 amejiua kwa sababu ambazo hazijatambuliwa.

Taarifa hizi zimesisitizwa na kiongozi wa kijiji cha Gaseke,Phocas Mvukiyehe ambaye amesema kwamba Anastase hakulala nyumbani kwake jana na kuwa mwili wake umepatikana katika shamba la jirani wake leo asubuhi akiwa maiti kama inavyokubaliwa na mke wake,Nyirasafari.

Pia,kiongozi wa eneo hili,Deogratias Seruvugo amesisitiza kwamba majirani wake wanasema kwamba malehemu aliwahi kujaribu kujiua miaka iliyopita na kuwa alikuwa anaishi kwa amani na majirani wake.

Seruvugo amesema”Tutapeleka mwili wake hospitalini ili kujua sababu ya kifo chake lakini kuna habari kwamba aliwahi jaribu kujiua miaka iliyopita”.

.Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top