kwamamaza 7

Nyabihu:Miaka nenda rudi yapita wakazi wakisubiri malipo ya mali iliyoharibika wakati wa mradi wa umeme

0

Wakazi wa kata ya Kareba, tarafa ya Mukamira,magharibi mwa nchi wametangaza kusubiri miaka sita malipo ya mali yao kama  miti iliyoharibika wakati wa ujenzi wa mradi wa umeme.

Mmoja wao amesema kuwa walitimiza mahitaji yote kama vile kufungua akaunti za benki kama walivyotakiwa na Kampuni ya EWASA (REG) lakini kuna waliolipwa baadhi ya wakazi  70

“EWASA ilikuja na kukata miti yetu ila hatujalipwa miaka sita imemalizika,hatujui kwa nini suala hili halitatuliwi,viongozi wa wilaya  na wa  kikao cha EWASA huko Mukamira,hawakutusaidia lolote”.

“Nilikuwa nikiuza mti kisha nikaweza kuitunza familia yangu,kulipa bima ya afya.Kwa sasa sijalipa karo,bima ya afya,tunahitaji msaada kwa kuwa tulisema tukachoka”.huyu ameongeza

Kiongozi wa wilaya ya Nyabihu,Theoneste Uwanzwenuwe ameeleza kuwa suala hili linajuliaka na kuwa linafanyiwa ufuatiliaji kwa kuwa orodha ya waliobaki ingali ofisini mwa EWASA(REG)

Wale ambao hawajalipwa hawakuwa na hati rasmi za kupata fedha zao wakati wa kulipa lakini mambo yote yameisha tayarishwa,EWASA(REG) ikipata uwezo itawalipa”.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Hata hivyo,Kiongozi wa REG wilayani Nyabihu,Alphonsine Nyirarukundo ametangaza  anafahamu kwamba hawa wakazi walilipwa fedha zao lakini ikiwa kuna suala kama hili kutafanyika ufuatiliaji

“Tutawasiliana na viongozi wa ngazi za chini huko ili kutatua suala hili”

Mradi wa umeme ulitimizwa eneo la Kareba mnamo mwaka 2013

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.