kwamamaza 7

Nyabihu: Matatizo yaliyoko kwenye jamii ndio anayofanya watoto kuacha shule

0

Wilaya ya Nyabihu kupitia Kiongozi wake Mtendaji, David anayejadili masuala ya elimu inatangaza kwamba idadi ya watoto wanaoacha shule imepungua kwa kiasi kikubwa kulingana na utafiti wa awali uliobainisha kwamba asilimia 5 ya wanafunzi wa shule za msingi na asiliamia 3 za wanafunzi wa shule za sekondali wamekatisha masomo.

Aliweka wazi kwamba mojawapo ya sababu inayowafanya kukatisha masomo yao ni matatizo ya kijamii yaliko katika familia zao yakiwemo matatizo ya lishe, utafutaji ajira kwa ajili ya kujipatia ruzuku, na hata ugomvi ndani ya familia na kufanya mtoto kutojisikia tulivu na hivyo kuacha shule.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Kiongozi huyu alibainisha kwamba pia kwa ajili ya kupambana na tatizo hili kumeweka mikakati kadhaa ya kuwarejesha shuleni. Ameonyesha kwamba kutatakiwa kampeni za kuwaelezea umuhimu wa kusoma kwa sababu kuna mojawapo ya wazazi ambao wangali na uelewa mbaya na hivyo hivyo tutaendelea na hasa kwa kufanya mikutano kwa kuieleza jamii umuhimu wa mambo ya elmu kwa mtoto.

Matokeo ya Utafiti uliofanywa kuhusu maisha bora ya familia wa mwaka 2013/2014 ulionyesha kwamba kiwango cha watoto wanaokimbia ama kukatisha masomo yao wanahesabiwa kwa asilimia 14 kwenye wilaya hiyo hiyo Nyabihu. Utafiti huu ulibainisha kwamba pia wale wenye miaka ya kusoma  wasiowahi kufika shuleni wanahesabiwa kwa asilimia 17.

Eneo hili linajulikana kuwa na idadi ya watoto wengi wenye miaka ya kusoma ambao hawafiki shuleni na hili lilimkera rais wa Rwanda alipoliizuru wilaya hii na kuwaona watoto wakizururazurura mitaani na hivyo kuwatupia lawama viongozi wa ngazi husika.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.