kwamamaza 7

Ningelipewa msaada na Uganda, ingelipinduliwa serikali ya Rwanda-  Jen. Kayumba Nyamwasa

0

Mpinzani mkubwa wa serikali ya Rwanda, Jen. Kayumba Nyamwasa amelaani mashtaka ya kuwa anapata msaada wa Uganda kupindua serikali ya Rwanda.

Jen. Kayumba alikimbia mwaka 2010 baada ya mazishi ya mama mzazi wake. Alisema hakuelewana na serikali nchini humo.

Kayumba ameambia chombo cha habari nchini Uganda, The New Vision kwamba madai kwamba Uganda inamsaidia katika mipango yake ya kupindua utawala nchini Rwanda ni uongo.

“Ningelipewa msaada  na Uganda, ingeipinduliwa serikali ya Rwanda.” Jen Kayumba amesema

“ Wanajua Uganda ilpokuwa ikiwasaidia, walipata ushindi hata kama wanakanusha hayo siku hizi.” Ameongeza

Kwa uande mwingine, Paul Kagame, Rais wa Rwanda, siku chache zilizopita alisema kwamba Uganda inasaidia chama chake Kayumba, Rwanda National Congress (RNC) kwa kulenga mashambulizi kwa nchi yake.

Hata hivyo, Uganda kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje, Sam Kutesa Kahamba ilikanusha madai ya Rais Kagame.

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.