HABARI MPYA

Nina ndoto za kurudi nchini Rwanda kama mfalme-Yuhi VI Bushaija

Yuhi VI Bushaija, 56, ametangazia The Sunday Times nchini Uingereza kuwa ana ndoto za kurudi nchini Rwanda kama mfalme.

Bushaija amesema kuwa alishangaa baada ya kusikia kuwa ndiye atakayechukua nafasi ya mfalme baada ya kifo cha mjomba wake,Kigeli V Ndahindurwa mwezi wa Januari 2017 nchini Marekani.

Kwenye mazungumzo haya,Bushaija ameleza kuwa hatakubali kumaliza milenia akiwa ukimbizini na kuwa ana ndoto za kurudi nchini Rwamda kama mfalme asiyekuwa wa ukimbizini.

Bushaija ameleza”Nina ndoto za kurudi nchini Rwanda kama mfalme asiyekuwa wa  ukimbizini siku moja”.

Pia ameongeza kwamba ataendelea kutii mila na desturi vya Wanyarwanda na kusaidia Wanyarwanda popote walipo.

Pamoja na haya,Bushaija ameonyesha upendo wake kwa familia ya ufalme wa Uimgereza Kupitia ujumbe alioutuma ili kumtakia mwanafalme Harry na mchumba wake,Meghan Markle kwa niaba ya wanyarwanda kwa kusema”Kwa niaba ya Wanyarwanda,nawatakia mema kwenye ndoa yenu.Ningetaka kuja kwenye harusi yenu lakini inawezekana kuwa kuna wageni wa kutosha”.

Yuhi VI Bushaija alifunga ndoa na mwanamke Lilian,49, walibalikiwa watoto watatu;msichana mmoja na wavulana wawili.Alizaliwa nchini Rwanda na kulelewa nchini Uganda alipohamia na kuenda Kenya kisha akaenda nchini Uingereza mwaka 2000.

Bushaija ametangaza kurudi nchini Rwanda kama mfalme wakati ambapo Rwanda ni Jamhuri tangu mwaka 1962.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook n

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top