kwamamaza 7

Ni uhalifu kumtukana Rais wa Rwanda- Mahakama Kuu

0

Mahakama Kuu nchini Rwanda imeamua ni uhalifu kumtukana Rais wa Rwanda.

Uamuzi huu ni baada ya mwanasheria Mugisha Richard kupiga rufaa akisema kusema maneno mabaya kuhusu rais haistahili kuwa uhalifu.

Ni kumaanisha kwamba atakayekuwa na hatia kwa hili atafungwa jela kati ya miaka tano kufika saba.

Kwa mwanasheria Mugisha jambo hili ni kinyume na katiba ya nchi na ni kipingamizi kwa haki za kujieleza.

Mahakama Kuu imesema sheria hii haitabadilika kutokana na wajibu wa ofisi ya urais.

Pia mahakama hii imepetisha sheria nyingine kwamba ni marufuku kuchora ‘cartoon’ za wabunge, mawaziri na wafanyakazi wengine wa serikali.

Pia mahakama imekataa vitendo vya uhasherati  kuwa ni uhalifu.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.