kwamamaza 7

Ni fimbo gani iliyopiga mchungaji na kondoo wakatawanyika

0

Kiongozi ni nani? Kiongozi ni mtu anayeongoza wengine. Kiongozi ni yule anayewatangulia wengine katika uwezo,upeo na hata namna yake ya kufanya yale yanayopaswa kufanywa. Kiongozi ni yule muwakilishi wa wengine wote katika kutimiza mambo katika jamii yake. Anaweza akawa hana ideas kubwa kuliko wengine lkn ni yuke ambaye anauwezo wa kujifunza haraka katika kufikia lengo lililowekwa. Anaaminiwa na kupewa majukumu kuliko wengine.

Mchungaji ni kiongozi. Biblia inawazungumzia wachungaji kwa namna mbili. Kuna namna wanaelezewa kama wanaochunga wanyama kama kondoo na mbuzi na kuna namna wanazungumziwa kama wanaochunga watu. Hii ya pili inahusisha kanisa na waumini. Ndipo mchungaji anaposimama kama muhimili wa kanisa. Aliyeaminiwa. Kama kiongozi au kichwa cha kanisa. Anakuwa Baba.

Shetani kwenye kiwango chake cha ubora anaijua vizuri kabisa methali isemayo “umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu”. Mambo mengi hutokea kwenye jamii hii iitwayo kanisa ambayo kwa macho ya damu na nyama tunaona kama ni mambo ya kawaida kabisa. Kuna nyakati tunaona ni kama ajali flani ( an accident) au imetokea tu kwa bahati mgongano (coincidence) lkn kwa macho ya rohoni ni zaidi ya yanavyoonekana. Vitu vyote vipo planned._

*Mathayo 26:31*
Ndipo Yesu akawaambia, Ninyi nyote mtachukizwa kwa ajili yangu usiku huu kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji, na kondoo wa kundi watatawanyika.

Yesu anaposema imeandikwa, anamaanisha alisoma kwenye kitabu cha nabii Zekaria.

*Zekaria 13:7*
Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema Bwana wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.

Ukitaka kuwapata watu na kuwatawala hakikisha unawakosesha mshikamano. Lete utengano kati yao. Pandikiza chuki. Ukifanya hayo hakuna lolote la maana litafanyika. Wakoloni walikuwa wana njia yao moja ya kutawala Afrika,wakiita *PLUNDERING AND LOOTING.* Walikuwa kwenye hiyo style wanawagombanisha ninyi wenyewe ili wapate kutawala. *Yani tenganisha kisha tawala.*

[xyz-ihs snippet=”google”]

Unakumbuka tulipokuwa darasa la 7B tulisoma mgogoro kati ya *Mangi Meri* na *Mangi Sina.* Mmoja alikuwa mmachame mwingine mmarangu. Walipogombana wao Wajerumani wakajiunga na mmoja wakampiga mwingine halafu walipomaliza hilo wakamgeuka huyu waliyenaye wakamchapa vizuri kwakuwa sasa alikuwa peke yake wakatawala. Simple arithmetic.

Chagua jina unalotaka iwe ni nabii,shemasi ,mchungaji,askofu,paroko,padre,nabii,mtume,mwenyekiti,katibu, mwalimu na majina mengine unayoweza kuyataja,wote hao wanaangukia kwenye group hili la MCHUNGAJI. Ni kiongozi. Wameaminiwa. Ni vile wanaongoza watu wengine wengi waliopo nyuma yao.

_Kwa siri sana watu hawa huwa na vita kubwa sana ambazo sio rahisi kuziona kwa macho yetu. Ndio sababu kama kanisa huwa tunatakiwa kuwaombea sana badala ya kuwacheka na kuwasimanga. Unajua ni kwanini?_

_Kiongozi anapopigwa na dhoruba flani naye akayumba,sio peke yake anayepotea. Timu yake yote hujikuta kwenye wakati mgumu. Shetani anapenda sana hili. Anakuwa amepiga jiwe moja ambalo limeuwa ndege wengi sana. Kwake ni Bingo._

Kwenye huu mtego wengi huwa tunaingia. Utasikia waumini wameanza maneno,”mchungaji mwenyewe mzinzi,mchungaji mwenyewe muongo,mchungaji mwenyewe hivi na vile..”na kila aina ya visingizio na maneno ambayo yanawafanya kuvunjika moyo kuchangia michango mbali mbali kanisani. Kujenga kanisa. Kuunda umoja imara. Kutoa sadaka. Kuhudhuria makongamano na semina au kushirikiana kwa namna yoyote kanisani na kubwa zaidi kushirikiana *NENO la Mungu.* Shetani hapo kusema Bingo kwa mara nyingine!

*Kwa shetani ni tofauti kumuangusha ndugu Kobelo Mwaifuge muumini wa kawaida tu kanisani na kumuangusha Stanley Kweka ambaye ni mzee wa kanisa. Au kumuangusha Kisa Mwaipyana ambaye ni mzee wa kanisa tu na kumuangusha Mchungaji Sebastian Matofali. Shetani anafaidi zaidi kuwapata wale tunaowaamimi na kuwapenda kuliko wale ambao si viongozi…. Anampiga mchungaji na kondoo wanatawanyika.*

Wapendwa,tujenge mazoea ya kuwaombea watumishi. Pale wanapopata dhoruba tusiwafanye topic za kuwaongelea vijiweni. Badala yake tuwaombee neema ya Mungu iendelee kuwafunika wapite salama. Tusiingie kwenye mtego ambao ni hasara kwetu wote kama kanisa. Siwatetei wao kufanya uovu kwa namna yoyote lkn kushikamana kwenye shida na dhoruba tunazopitia ni msingi wa kuvuka salama. Ni rahisi kuvuka salama tukiwa wengi kuliko wachache…. Utengano ni udhaifu.

_Lkn umoja hauwezi kuwapo kama hakuna Upendo. Upendo ukiwapo kati yetu tutasimama pamoja,tutalia pamoja na kushangilia pamoja. Wakati Yesu anawaambia hayo maneno alijua shetani atawapepeta na watatawanyika. Lkn Yesu aliwapenda tu. Anawaambia,ingawa mtanisaliti na kutawanyika “mimi nawatangulia kwenda Galilaya”._

Leo moja ya matatizo mengi tuliyonayo ni dhahiri kuwa ni kukosekana umoja. Kila mtu anafanya lake kwa sababu zake. Inaweza kuwa kuinua jina. Utukufu binafsi na mambo mengine ambayo si ya kuimarisha umoja wetu. Lkn umoja hauwezi kuwapo kama hatuna Upendo. Kumthamini kila mtu. Kuchukuliana. Kuvumiliana. Kutohesabiana mabaya. Kufadhiriana na zile tabia nyingine zote za Upendo kama tuzijuavyo kutoka kitabu cha Wakorintho.

*1 Wakorintho 13:4-7*
Upendo huvumilia, upendo hufadhili; upendo hauna wivu au majivuno.
5 Upendo hauna kiburi na haukosi kuwa na adabu. Upendo hau tafuti kujipendeza nafsi; haukasiriki upesi, hauweki orodha ya mabaya. 6 Upendo haufurahii mabaya, bali hufurahia kweli. 7 Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahim ili yote.

Vitu vingi haviendi kwenye jamii zetu kwakuwa tayari wachungaji wameshapigwa na kondoo tumebaki bila mchungaji na tumetawanyika. Mchungaji anaweza kuwa mchungaji, mwenyekiti,parish worker, mwinjilisti, katibu,shemasi,mzee wa kanisa,kiongozi wa jumuiya nk. Mbaya zaidi sisi kondoo. Tunatumia hisia kuikabili hii hali badala ya kuomba neema na hekima ya Mungu. Mstari wa 33 Petro anatumia hisia zake kama sisi. Msikie.

*”Wajapochukizwa wote kwa ajili yako,mimi sitachukizwa kamwe”.*

Wanyakyusa wanasemaga ” mbombo ngafu”. Yani kazi ipo au kazi sana. Kama mambo ya rohoni yanashughulikiwa kwa hisia(mwili) lazima iwepo kazi. Hatari sana. Petro huyo huyo anayetoa maneno ya kishujaa hapo akamsaliti Yesu muda mfupi baadaye. Mambo ya rohoni hayashughulikiwi kimwili.

Hao “wachungaji”wakipigwa wengi wetu huwa tunapata sababu za kufanya isivyotakiwa kwakuwa hao hawajawa mfano kwetu. Tuliwaamnini na sasa wamepoteza uaminifu eti. Badala ya kuwaombea tunawasimanga na kuwacheka. Tunasahau kuwa vita ya mchungaji huwa ni kubwa kuliko yako.

Wewe kama umeamua kuangusha laana zako angusha kama wewe. Usitafute visingizio. Ukiamua kulikoroga likoroge on your own usitafute excuses. Fanya weusi wako kwakuwa umeamua kufanya na sio kuwasingizia watu flani. Msafi azidi kujisafisha. Na muovu zaidi kujichafua. Wala hakuna anayekusababisha ufanye hayo. Ni wewe mwenyewe na utashi wako. Sio mchungaji wala shemasi. Sio parish worker wala nabii..hiyo ni wewe mwenyewe. Chochote kizuri unachoacha kukifanya ni kwa sababu umeamua kama wewe kutokifanya. Usitafute sababu. Kila mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe siku ya hukumu*

Mbarikiwe.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Leki@bwiza.com

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.