kwamamaza 7

Ngororero: Wazazi waahidi kuanzisha idara ya masomo ya Uchimbaji migodi

0

Wazazi wanaosomeshea watoto wao katika Gatumba Technical Secondary School, shule liloko katika wilaya ya Ngororero, wasema kwamba wana mpango wa kuanzisha idara ya masomo ya uchimbaji migodi kwa ajili ya kupambana na uchimbaji migodi wa bila mpango na vifo vinavyohusiana na suala hii vinavyojitokeza bado katika wilaya hii.

Wazazi wanaosomesha watoto katika shule hili, wameahidi katika mkutano wao mkuu, uliofanyika 17/06/2017, kwamba wako tayari kufanya kila juhudi ili kuanzisha idara hii ya masomo ya uchimbaji migodi.

Nikobasanzwe Gerald Ntwari, Mwenyekiti wa Kamati ya wazazi katika shule la Gatumba Technical Secondary School, amesema kwamba walikuja na wazo hili baada ya kuona wingi wa migodi katika wilayani hii, na watu huwa wana hatari ya vifo kulingana na uchimbaji usio wa kitaaluma.

“Unajua hatutakiwi kutegemea serikali kufanya kila jambo, na sisi tunapaswa kuchangia. Tutafanya kila juhudi kuwatafuta wataalam wa sekta hii, ili waweze kusomesha watoto wetu na hii itasaidia kutoa wafanyakazi wa uchimbaji migodi wenye elimu inayohitajika na kuondoa uchimbaji usio na mpango”

Mzazi huu alisema pia kwamba juhudi zao zitalenga kuwapa elimu inayowawezesha kuvuka mipaka ya Rwanda na hata kupatia suluhu tatizo la ukosefu wa ajira.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ugirinshuti Jean d’Amour, Mkurugenzi wa shule hili alisema kwamba walishtuka kwa pendekezo la wazazi hawa kwa sababu shule lilikuwa katika majadiliano na idara ya WDA, na akaamini ni ishara kwamba kutekelezeka kwa mpango huu kutawezekana mapema.

Na hata wanafunzi waliupokea mpango huu kwa shangwe, Ndagijimana Jean de Dieu mwanafunzi wa darasa la tano alisema kwamba watajaribu kuwahimiza wadogo wao kuja kufuata masomo haya ya Uchumbaji migodi kwa kuwa katika wilaya yao wana hazina ya migodi mingi.

Mkurugenzi wa masuala ya elimu katika wilaya, Niyonsenga Protegene, alisema kwamba ni mchango mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya wilaya, na aliwaahidi wazazi kuwa uongozi wa wilaya utafuatilia kwa karibu na kutoa msaada kadiri utakavyohitajika.

“Tuna hazina ya migodi mingi, lakini kuizalisha mali imekuwa ni tatizo kwa sababu ya kutokuwa na watu wenye ujuzi unaohitajika. Kwa sasa kutokana na mchango wa wazazi, itatusaidia kuiendeleza wilaya na hata raia wake” asema

Shule hili lenye wanafunzi 500 ambalo lilifungua milango mwaka 1988, linasomesha masomo katika mikondo ya Ujenzi na Umeme. Kuanzishwa kwa masomo haya kunalingana na mfumo wa serikali unaowahimiza watu kufuata kwa wingi masomo yenye ujuzi wa kutenda yatakayowawezesha wahitimu kujiajira mara baada ya kumaliza masomo yao kwa ajiri ya kupambana na ukosefu ajira.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

 Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.