kwamamaza 7

Nchi wanachama wa UA zilishawishika na mfumo wa kijifadhili – Ripoti ya Rais Kagame

0

Rais kagame alihotubia katika kikao cha Muungano Wa Afrika(AU) akifafanua ripoti waliyoifanya kuhusu mageuzi na  mfumo wa Kujifadhili wa AU kupitia  nchi wanachama iliyokuwa ikilenga mfumo wa  kuepukana na tabia ya kutegemea ufadhili kutoka nchi za magharibi.

Katika ripoti hii kuhusu mageuzi ya AU kulipendekezwa nchi zichangie asilimia 0.2 ya bajeti yao kama matokeo ya ripoti ya ripoti hii anavyoeleza.

Nchii hizi zinazojumuika katika Muungano wa Afrika zimekwisha anza kuona kwamba mfumo huu wa mageuzi na hata tabia ya kujifadhili vimeanza kuzaa matunda na kueleweka kwa baina ya nchi wanachama wa Muungano huu.

Mpaka sasa 1/5 ya nchi wanachama wa Muungano huu zimekwisha toa mchango wao na zimejidalilisha kuupokea kwa shangwe na kuonyesha hali ya kuusifia Muungano huu. Mfano wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aliyeonyesha sheki ya mchango wa nchi yake ya milioni moja ya dola za Marekani 1,000,000 USD fedha ambazo zilitokana na mauzo ya ng’ombe wanaofugiwa nchini mwake.

Rais Kagame akigusia nia ya nchi kuchangia katika Muungano huu alisema kwamba ni ishara kwamba malengo ya Muungano huu yatafikiwa.

“Kwa kuwa 1/5 ya nchi wanachama zimekwisha toa mchango wao wa kufadhili katika bajeti ya Muungano huu ambao unapaswa kuwa 0.2 ni ishara kwamba malengo ya kujifadhili yanawezekana sana” asema rais wa Rwanda Kagame.

Akigusia kuhusu faida ya mageuzi haya rais Kagame amesema kwamba na hata wale ambao wanataka kuikata moyo Afrika wangekoma wakiona Afrika inafanya mambo yake kwa kujitegemea na mipango yake  kwa njia nyororo.

Viongozi tofauti akiwemo rais wa Zimababwe Robert Mugabe, waliomba wanashirika wa Muungano huu kuchangia kuujenga Muungano huu kwa misingi imara.

“Mwache tujijengee Muungano huu, kidogo kidogo, hatua kwa hatua na tutaifiakia mwishowe Afrika ya ndoto zetu” asema Robert Mugabe

Mwenyekiti  wa Tume ya Muungano huu, Mousa Fataki aliahidi wanachama kuichunga miradi na mali ya muungano huu ipasavyo.

Kikao hiki ambacho kimefanyika Addis Ababa tarehe 3 Julai kilikuwa kinafanyika kwa mara ya 29 ambapo cha awali kilikuwa kimefanyika mjini Kigali mwezi Januari ambako rais Kagame alipewa jukumu la kikiongoza kikosi ambacho kilikuwa kikishughuliakia mageuzi ya Muungano huu.

bonyeza hapa kupokea gazeti juu ya facebook juu ya twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.