kwamamaza 7

Nawatakia heri na fanaka-Yuhi IV Bushaija

0

Kupitia barua yake fupi, anayedai kuwa ni mfalme wa Rwanda,Yuhi IV Bushaija  Emmanuel,56, amewatakia Wanyarwanda amani na kuwaomboleza walioikuta misiba mbalimbali mwaka jana,2017.

Yuhi IV Bushaija amewakumbusha Wanyarwanda kwamba umoja ni nguvu na kuwa haina budi kuzingatia na kutekeleza jambo hili kupitia upendo na ushirikiano.

Yuhi IV Bushaija ameshauri “Yaliyopita si ndwele tungoje yajayo,inabidi ushirikiano,tupige marufuku chuki na uchonganishi wowote ili kuishi amani”.

Hili ni baada ya Yuhi IV Bushaija kutangazia The Sunday Times nchini Uingereza kuwa ana ndoto za kurudi nchini Rwanda kama mfalme.

[xyz-ihs snippet=”google-pub”]

Yuhi IV Bushaija alichukua nafasi ya ufalme baada ya kifo cha mjomba wake,Kigeli V Ndahindurwa mwezi  Januari 2017 nchini Marekani.

Yuhi IV Bushaija Emmanuel alizaliwa nchini Rwanda na kukua akiwa nchini Uganda alipohamia na kuenda nchini Kenya baadaye akaenda nchini Uingereza mwaka 2000.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook n

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.