kwamamaza 7

Nadhani haiwezekani- Kagame  afunguka kuhusu vita na Uganda

0

Rais Kagame Paul wa Rwanda ametangaza haiwezekani uwepo wa vita kati ya Rwanda na Uganda hata kama kuna msuguano kati ya nchi mbili.

Miaka miwili imemalizika kukiwa ushirikiano usio mzuri kati ya Rwanda na Uganda.

Kagame ametangazia gazeti la TAZ jana kuwa  nchini Ubelgiji.

“ Watu wanaogopa vita kati yetu. Nadhani haiwezekani kwani Uganda ina jua bei yake. Hatutaki kutumia njia hio kwa kuwa kila yeyote atapata hasara,” Kagame amesema

“ Kuna raia wetu ambao ni wafungwa nchini Uganda. Ni Wanyarwanda wengi ambao wangali gerezani. Maelezo ya Uganda kuhusu hili hayabadiliki. Wanasema walingia nchini humo kinyume na sheria, kwamba ni wajasusi.” Ameongeza

Pamoja na hayo, Rais Kagame amesema waliasiliana na Uganda kuhusu suala hili lakini Uganda haikufanya lolote hata kuwafikisha mahakamani.

Amesisitiza Uganda itafanya lolote itakalo lakini haitakuwa sawa kwa kuvuka mpaka.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.