HABARI MPYA

Mtuhumiwa wa mauaji ya muimbaji Mowzey Radio afungwa muda kizuizini

Mwanamume Godfery Wamala maarufu kama Troy ambaye anatuhumiwa kumuua muimbaji Moses Ssekibogo Nakitinje maarufu kama Mowzey Radio jana amesimama kizimbani na kufungwa muda kizuizini hadi tarehe 26 Februari 2018.

Jaji mkuu wa mahakama ya Entebbe,Mary Keitesi Lukwago amefafanua kwamba uamuzi huu ni kutokana na kuwa mshitakiwa anatuhumiwa uhalifu wa kiwango cha juu ambao unastahili kuhukumiwa katika mahakama kuu.

Chimpreports imeeleza kuwa pia uamuzi huu umechukuliwa  baada ya mwanasheria wa serikali,Julius Muhiirwe kutangaza kwamba polisi haijamaliza kufanya upelelezi husika na kesi hii.

Godfrey Wamala ni mkazi wa Nsangi,wilayani Wakiso mjini Kampala,alikamatwa na plisi wiki iliyopita kwa kutuhumiwa kumuua muimbaji Mowzey Radio kwa kumpiga waliopokuwa baani ‘De Bar’ eneo la Entebbe.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top