kwamamaza 7

Msemaji wa chama cha Jenerali Kayumba Nyamwasa kusimama kizimbani pamoja na Diane Rwigara

0

Mahakama kuu mjini Kigali nchini Rwanda imetangaza kuwakamata watu wanne  wakiwemo msemaji wa Chama cha upinzani kwa serikali ya Rwanda(Rwanda National Congress),Jean Paul Turayishimiye ambaye anaishi Marekani.

Inatarajika kwamba mbali na Turayishimiye, watakamatwa wengine wakiwemo Thabita Mugenzi(Shangazi wa Diane Rwigara),Xaverine Mukangarambe na Edmund Musheija ili kusimama kizimbani pamoja na  Diane Rwigara anayeshtakiwa mashtaka yakiwemo uchochezi.

Jaji Ndibwami alitoa ombi hili jana tarehe 7 Meyi 2018  lakini wanasheria wa watuhumiwa Me Gatera Gashabana(Adeline Rwigara) na Me Buhuru Celestin(Diane Rwigara) wamekanusha hili kwa kusema litachelewesha kesi ya wateja wao.

Mwendeshamashtaka amefafanua hawa watu wane watakamatwa kwani  waliwaunga mkono Diane Rwigara na mama yake Adeline Rwigara kwenye uhalifu wa uchochezi kupitia mazungumzo kati yao hasa kupitia mitandao ya kijamii.

Ikumbukwe kwamba mwaka jana 2017, kulitiwa hadharani sauti zilizosemekana kuwa zilipitia Whatsupp ambako alisikika Adeline Mukangemanyi  akizungumza na hawa watu wanne wakikosoa serikali ya Rwanda.

Kwa sasa,haijaeleweka kama mahakama itaanzisha mpango wa kuwafikisha mahakamani kwa kuwa wote wanaishi ugenini kama vile Marekani,Canada na Ubelgiji.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song update

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.