kwamamaza 7

Mpayimana yaidhinishwa na NEC huku wagombea Rwigara, Mwenedata na Barafinda wakikataliwa

0

Baada ya Tume ya Uchaguzi ya Rwanda (NEC) kuwatangaza wagombea rasmi wagombea tatu mwa sita waliowasilisha nyaraka zao kwa tume hiyo ndio waliowahi kuidhinishwa huku Diane Rwigara, Mwenedata Girlbert na Barafinda Fred kukataliwa kuidhinishwa kama wagombea.

Wagombea ambao waliwahi kuidhinishwa kwa mjibu wa tangazo la Tume ya Uchaguzi la Ijumaa tarehe 7 Julai ni Mh. rais Paul Kagame, Dkt. Frank Habineza na Mpayimana Phillipe ambaye ni mgombea huru pekee.

Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Tume hiyi Prof. Kalisa Mbanda , makamishna wa Tume hii ya Uchaguzi kuzichunguza nyaraka za wagombea hao wote waliokataliwa wengi wao walikabili kutojaza nyaraka zao hususani saini za wafuasi.

Kuhusu  Rwigara Diane aliwahi kupata saini za wafuasi wapatao 572 mwa 600 ambao ni sharti kutolewa. Kwa kuchunguza orodha za wafuasi walipatikana mojawapo ya 3 watu ambao waliofariki. Sababu nyingine iliyomfanya kutokubaliwa ni kupatikana na kosa la kuiga saini za watu 26 wa wilaya ya Rulindo kwa kushirikiana na mfanyakazi wa kujitolea wa Tume ya Uchaguzi anayetambulika kwa jina la UWINGABIRE Joseph.

Kuhusu Barafinda Fred, hakujaza saini za wafuasi ambapo aliwahi tu kupata saini 362 mwa 600 zinazohitajika . Hakuikabidhi Tume ya Uchaguzi kitambulisho cha uraia wa asili, na hata uraia wa asili wa mmoja ya wazazi wake.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mwenedata Gilbert naye hakujaza idadi ya wafuasi wanaohitajika kwa kuwa aliwahi tu kupata saini 522 mwa 600 zinazohitajika. Naye kwa kuchunguzwa kwa saini zake alipatikana na mtu mmoja aliyefariki mwenye asili ya wilaya ya Gatsibo.

Baada ya Tume hii kuwatangaza wagombea rasmi inatarajiwa shughuli za kampeni kwa wagombea hawa watatu  kuanza hapo tarehe 14 Julai ambapo zitamalika tarehe 3 Julai huku uchaguzi mkuu ukitarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 mwezi ujao.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.