kwamamaza 7

Mnyarwanda mjamzito afariki akijaribu kuingia nchini Uganda

0

Mwanamke mja mzito raia wa Rwanda, Elisabeth Mukarugwiza ameaga dunia wakati akijaribu kuingia nchini Uganda kupitia njia za vichochoro.

Kisa hiki kimetokea jana tarehe 23 Machi kwenye mpaka wa Rwanda na Uganda, Cyanika ambako Mukarugwiza, 39, alikimbizwa na watu ambao hawakujulikana na kuanguka chini na kwa hili, akafa hapo hapo.

Kwa mujibu wa taarifa za Chimpreports, malehemu ni mkazi wa Wilaya ya Musanze, Kinigi,mkoa wa Kaskazini mwa Rwanda na alikuwa anataka kwenda nchini Uganda kutafuta chakula na matibabu.

Taarifa hizi zinasema mwili wa Mukarugwiza umerudishwa nchini Rwanda kuzikwa.

Kifo hiki kimekuja baada ya viongozi mbali mbali nchini Rwanda kuwashauri wananchi kutokwenda nchini Uganda kutokana na hali ya usalama wao ambayo haiko vizuri.

Rwanda inashtaki Uganda kuwanyanyasa raia wake, jambo ambalo Uganda inalaani kwa kusema wanaokamatwa ni watuhumiwa wa uhalifu kama vile mambo ya kuharibu usalama.

Hata hivyo, viongozi wa Rwanda hawajafunguka lolote kuhusu hiki kisa.

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.