kwamamaza 7

Mnyarwanda bi Jen. Kale Kayihura akamatwa

0

Bi Jen. Kale Kayihura Angela Kayihura anayedaiwa kuwa Mnyarwanda amekamatwa.

Taarifa za  Spyreports zimeeleza Angella Kayihura amekamatwa kutoka nyumbani kwake Muyenga mjini Kampala  na kupelekwa mahali pasipojulikana kwa sasa.

Hiki chombo cha habari kimeeleza hakikuweza kuwasiliana na  msemaji wa jeshi la Uganda Brig. Richad Karemire kuhusu hili suala.

Kwa sasa haijaeleweka waziwazi kama Angella amekamatwa kwa mashtaka sawa  na ya mumewe aliyekamatwa jana.

Kuna taarifa ambazo hazijakamilishwa kama Angella alikuwa akiwasiliana na wapelelezi wa nchi za nje ambazo hazikutajwa.

Angella Kayihura na Kale Kayihura walizaa watoto wawili; Tesi na Kale Jr.

Inadaiwa kuwa Angella ni mtoto wa kizazi cha mfalume wa mwisho wa Rwanda, Mutara III Rudahigwa.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.