kwamamaza 7

Mnyarwanda aondolewa kucha za miguu nchini Uganda

0

Mnyarwanda, Venant Musoni Hakorimana, 35, alifika nchini Rwanda Ijumaa baada ya kufungwa na kuteswa kimwili  hadi aliopondolewa kucha za miguu gerezani nchini Uganda.

Musoni ametangaza kuwa alikuwa akipigwa kila siku kwa kutumia nyaya za umeme.

“ Sikuweza hata kusimama, kwa kuanguka, mwanajeshi alikuwa akiniamsha kwa mateke. Wanawanyanyasa watu.Kumfunga fulani mwaka na nusu bila hatia ni kosa.” Amesema Musoni

“ Kulikuwa Wanyarwanda wengine kama 40 chumbani kidogo. Nakumbuka mmoja, Nelson Mugabo ambaye alipigwa kiasi ambacho hawezi kwenda kwa miguu.” Ameongeza

“Unaweza kujua ukweli bila kumpiga mtu kiasi apoteze fahamu na kuzirai.” Ameshauri

Pamoja na hayo, Wanyarwanda walishauriwa kutokwenda nchini Uganda. Ni baada ya wengi kukamatwa, kuteswa kimwili na kupokonywa mali zao.

Msuguano kati ya Rwanda na Uganda ulianza miaka miwili iliyopita. Uganda inashtaki Rwanda upelelezi, mashtaka ambayo inalaani mno.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.