kwamamaza 7

Mnyarwanda aliyepigwa risasi akingia nchini Uganda afunguka

0

Mnyarwanda Innocent Ndahimana aliyepigwa risasi na Polisi ya Rwanda akijaribu kuingia nchini Uganda kupitia Mpaka wa Gatuna, kaskazini nchini humo amesema alikuwa akitafuta kuuza maharagwe kilo 500 kwa bei nzuri.

Ndahimana ameambia Daily Monitor kwamba alipinga amri ya polisi kuingia nchini Uganda kisha akapigwa risasi.

“  Afisa wa usalama aliniamru kusimama, sikufuata amri yake kwani bei ya maharagwe nchini Uganda kwa kilo ni Shilingi 2350 na Rwanda ni 200 tu.” Amesema Ndahimana

Amesema alipopigwa risasi aliangukia upande wa Uganda na wenzake wakampeleka nchini Uganda kutibiwa.

Anayemtibu, Alex Niwahereza amesema Ndahimana ameanza kupona na anaweza kurudi kwao.

Hata hivyo, huyu anaogopa kuwa atakamatwa atakaporudi nchini Rwanda kwa kuwa alibeza sheria.

Pamoja na hayo, Wanyarwanda walishauriwa kutokwenda nchini Uganda. Pengine, inaonekana waizwazi kuwa Wanyarwanda hawakuzingatia ushauri huu halafu wanakwenda nchini humo kutafuta bidhaa mbali mbali kwa bei ndogo na ya humo nchini Rwanda.

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.