Warembo 16 waliokuwa wanashiriki shindano la kumtafuta Miss Burundi 2018 wamejiondoa katika hatua ya fainali  wakidai kuna uongo wa zawadi itakayotolewa kwa washindaji.

Kupitia barua waliyoandika, hao wamedai kuwa kuna udanganyifu mkubwa kwenye zawadi atakayotunukiwa mshindi wa kwanza na wa pili.

Wandaaji wa shindano hilo, Bujumbura events awali walisema kuwa mshindi angejinyakulia gari jipya pamoja na kiwanja chenye ukubwa wa mita mraba mia nne na tuzo ya pesa taslim swala ambalo wasichana hao wanadai hakuna kilichoandalaliwa kwa ajili yao mpaka sasa.

 

 

Barua waliyoandika warembo wa Burundi

Fainali hiyo ambayo ilipangwa kufanyika tarehe 21 Julai 2018, ime ahirishwa na wandaaji wa shindano hilo na kusogezwa mbele hadi Julai 28.

Tukio hili limezusha hofu la  mlimbwende  ambaye atawakilisha nchi hiyo kimataifa kwa mwaka huu wa 2018.

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

ACHA JIBU

Tanga igitekerezo
Andika amazina

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.