HABARI MPYA

Mimi ngali hai,sijakufa-Faustin Twagiramungu

Mwenyekiti wa chama cha upinzani RDI-RWIZA,Faustin Twagiramungu amekana taarifa zilizosema kwamba aliaga dunia na kuwa atafanya ufuatiliaji ili kujua asili zake.

Wikipedia inaonyesha kwamba Twagiramungu alifariki mwaka 2017

Kupitia BBC,Twagiramungu ametangaza kwamba yeye ni hai na kuwa ataendelea na kazi zake za kisiasa.

Mimi ni hai,pamoja na mungu naamini kuwa nitadumu”ametangaza Twagiramungu.

Mwanasiasa huyu ametangza kwamba hajui chanzo cha taarifa za kifo chake kama inavyonekana kwenye Wikipedia na kuwa atafanya ufuatiliaji wake ili kujua chimbuko.

Faustin Twagiramungu,72, anaishi mjini Bruxelles,Ubelgiji ni mzaliwa wa Cyangugu kusini magharibi mwa Rwanda.

 

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top