kwamamaza 7

Mfumo wa kudhibiti kesi wa Rwanda kuunganishwa na saini za Kieletroni na alama za vidole

0

Mfumo huu wa Kieletroniki wa Wizara Sheria unaoeleweka kama Mfumo wa Pamoja wa Kielektroniki wa Kudhibiti Kesi kwa upine wa maneno ya Kingereza (IECMS) unatarajiwa kutunukiwa zawadi katika mifumo ya kieletroni kumi bora ya dunia kwenye kikao cha kila mwaka cha Shirika la Taifa la Kuhifadhi Kesi (National Association for Court Management) mjini Washington,DC.

Mfumo huu wa IECMS ambao utatunukiwa leo umechaguliwa na shirika hili kama mjawapo ya mifumo ya ngazi za sheria za kudhibiti kesi uliofauru kwa mjibu wa gazeti la The New Times la Rwanda.

Ni mfumo ambao uliunganishwa na taasisi nyingi zinazohudumu kielektroniki kama Chuo cha Vitambulisho Mamlaka ya Kodi ya Mapato ya Rwanda (RRA), na Idara ya Ardhi.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Iko mipangoni maafisa kwa ajili ya kuuongezea nguvu mfumo huu kuunganisha rekodi zake na saini za watu na hata alama za vidole na hii itamaliza bila shaka kutumia karatasi kwa hapa na hapa.

IECMS ni mfumo ulioanzishwa na wizara ya sheria utategemewa kuwa suluhu kwa kuchelewa, kupeleka peleka kesi na ilikuwa pia inalenga kuunganisha kupatikana kwa  haki kwa kuziunganisha taratibu zote kuanzia kuchunguzwa kwa kesi hadi mtu kwenye ngazi ya kutumika kifungo.

Waziri wa Sheria Jonhston Busingye alionyesha kufurahia zawadi hii na kwa kukumbusha kuwa mfumo huu ulianzishwa ili kufanikisha mfumo wa kielektroniki  wa mahakama.

“unatumika nchini mwote kwenye mahakama zote majiji na waendesha mashtaka wote wa Rwanda wanautumia. Kutunukiwa kwake inatutia moyo wa kuongezea nguvu na kuuboresha” asema waziri

Waziri aliusifu pia mfumo huu kwa kuwa unaendesha kazi kwa haraka na kuhamasisha kutolewa kwa haki na hugharimu fedha ndogo.

Mfumo huu kwa sasa unawawezesha wananchi kufuatilia kwa karibu kesi zao bila kupoteza muda na kupoteza chochote na wakapokea taarifa maalum kuhusu kesi zao wakiwa tu nyumbani kwao.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.