Connect with us

DINI

Mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi:Klezia katoliki haikuomba msamaha kamili- aliyekuwa padri, Jean Ndorimana

Published

on

Aliyewahi kuwa padri wa klezia katoliki,Jean Ndorimana,65 amesisitiza kwamba klezia katoliki nchini Rwanda iliomba msamaha nusu kuhusu madhambi iliyoyafanya wakati wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mnamo mwaka 1994.

Alipokuwa kuwa akizungumza na Jeune Afrique,kwa sauti yenye masikitiko Jean Ndorimana aliyekuwa padri kuanzia mwaka 1980 hadi 2009 amehoji kwamba klezia katoliki haina budi kuomba msamaha kamili  Wanyarwanda kwa ujumla.

Jean Ndorimana amendelea kwa kusema kwamba mwenye utakatifu papa Francis alishauriwa na Mgr Gieuseppe Bertello kuomba msamaha kwa niaba ya klezia katoliki.

Pia,ameongeza kwamba ziara ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame ilisaidia mno wakatoliki nchini Rwanda kwani Papa Francis aliwonyesha kwamba kulikuwa kasoro kwenye msamaha waliwouomba maskofu wa Rwanda.

Pengine,Ndorimana amesisitiza kwamba klezia katoliki haikstahili kusubiri miaka 22 ili kuomba msamaha na kuwa itabidi baraza kuu la maskofu kueleza kinagaubaga kuhusu barua ilioandikwa ikisema kuwa kulitokea mauaji ya kimbali mawili nchini Rwanda.

Jean Ndorimana alikuwa padri,hakukubaliana na maskofu mbalimbali baaada ya kuweka wazi maandishi husika na madhambi ya klezia katoliki wakati wa mauaji ya kimbali dhidi ya Tutsi mwaka 1994.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Advertisement
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *