kwamamaza 7

Matumaini ya kushinda uchaguzi yanalingana na mipango tunayoweka mbele –RPF

0

Chama cha RPF Inkotanyi chasema hakina ushindani wa maneno juu ya atakaeshinda uchaguzi bali tu kinaweka kipaumbele yale kitakawaletea wanyarwanda baada ya kushinda uchaguzi.

François Ngarambe,katibu Mkuu wa chama cha RPF Inkotanyi ametangaza haya alipokuwa katika mahojiano na waandishi wa habari na alibainisha kwamba wanyarwanda wangetarajia mengi katika muhula wa miaka 7 mbele.

Waandishi wa habari walimwuliza pia ikiwa hawana mashaka watashinda uchaguzi kwa kuwa na hata wapinzani wao wanajigamba kuwa watawashinda katika uchaguzi wa rais wa  hapo mwezi ujao.

“hatuna hofu yoyote ya kuwa tutashinda uchaguzi au la, bali tunacho tia maanani ni mipango tutakayofanya kwa ajili ya wanyarwanda” asema katibu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

“hatujali washindani, tunachojali ni mipango ambayo tutawaletea wanyarwanda nao wakafanya uamuzi wao. Ila sitasema tuna imani ya kushinda kwa asilimia 100 tuna mipango ya kueleweka na inalingana na mwelekeo wa wanyarwanda. Hatujasema huyu ni mshindani wa kutisha mbele yetu tunachotia maanani ni mipango tuliyo nayo na hata mgombea wa tiketi yetu ambaye ni rais Paul Kagame, kwa hiyo ni zamu itakuwa ya wapiga kura kufanya uamuzi” François Ngarambe.

Chama cha RPF kinakwenda uchaguzi kikiwa na wagombea wapinzani wawili ambao ni Frank Habineza wa chama cha Green na hata Mpayimana Phillipe ambaye ni mgombea huru pekee aliyeweza kuidhinishwa na Tume ya Uchaguzi.

Baada  ya wagombea rasmi kutangazwa tarehe 7 Julai shughuli za uchaguzi zinaendelea na kampeni kwa wagombea, ambako wagombea watakuwa wakieleza mipango yao kwa wanyarwanda wenye umri wa kushiriki uchaguzi huku wakijaribu kutafuta kura. Shughuliza za kampeni zinatarajiwa kuanza hapo kesho tarehe ya 14 na kumalizika tarehe 3 Agosti ambayo ndiyo tarehe ya kuanza uchaguzi kwa wanyarwanda wanaoishi Diaspora na 4 Agosti kwa wanyarwanda wa ndani.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.