kwamamaza 7

Matokeo ya Uchaguzi anajulikana tangu Oktoba 2015- Rais Kagame

0

Haya ni maneno ya Rais Kagame ambaye ni mgombea kwa tiketi ya chama cha RPF wakati alipokuwa katika shughuli za kampeni yake ambazo zimeanza leo hii tarehe 14.

Rais Kagame amepokewa na raia chungu nzima wa wilaya ya Ruhango ambao wamekuja kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Ruhango kuhudhuria hafla hii na kumwonyesha kwamba wanamwunga mkono katika kinyang’anyiro cha muhula wa tatu wa urais wa Rwanda.

Mfuasi wa chama cha RPF Bw Ndamyuwera Jean Sother, amesifu ambayo aliafikia yote kwa kuweko kwa utawala wa RPF Inkotanyi unaoongozwa na Paul Kagame na kutoa wito kwa raia wa wilaya ya Ruhango wote kumpa kura rais Kagame katika uchaguzi wa hapo mwezi ujao.

Rais Kagame naye alifuata katika hotuba yake ambapo alianza kwa kuwashkuru vyama vya siasa vilivyojijumuisha na kumwunga mkono rais mgombea wa chama cha RPF ambaye ndiye mwenyewe Rais Kagame.

“Nawashkuru ninyi wote viongozi wa vyama na wanachama wanu mbalimbali mliko hapa, RPF ilileta umoja mwa wanyarwanda, wanyarwanda wanaishi kwa umoja, nchi moja tuna kitu cha kutuunganisha ambacho ni kwamba unyarwanda na kujenga nchi yetu”

Naishkuru RPF kwa kuwa na Imani yake pekee na hasa kwangu.

“Waandishi wa habari huwa wanaandika eti matokeo ya uchaguzi yanajulikana , ni kweli nawapongeza kwa kujuwa hivyo, matokeo ya uchaguzi yalikwisha fahamika mwezi Octoba wa mwaka 2015 wakati ambapo mamilioni ya watu walipeleka nyaraka zao kwa bunge wakiomba kura ya maoni ambayo kwa kura ya maoni iliidhinishwa kwa asilimia karibu 100.”

Mipango aliyoiweka mbele inajumuika na kuendeleza kwa kasi yaliyokwisha fikiwa.

Aliwaelezea kwamba wanataka Kuendelea kuongeza yaliyokwisha fikiwa na kuyajumlisha, kwa kusambaza umeme mahali pote, kujenga shule nyingi, watoto wakasoma.

Kujenga sekta ya afya iliyo na msimamo imara kwa kuhakikisha kwamba wanyarwanda wanapata afya bora.

Kujenga barabara, na kuwa na shughuli mbalimbali za kujiendeleza, watu wakamudu shughuli kama hizo, wakafanya biashara na kushirikiana na kuasiliana na mataifa kibiashara na mengineyo yatakayoweza kuwatajirisha wanyarwanda.

Usalama kwa wanyarwanda, umoja na haki ya kuwa kile ambacho ni ndoto ya fulani bila kuvunja haki ya yeyote, hayo yote yana pia mwendo fulani ambao ndio tunaoufuata, tunataka kusonga mbele na kubadilisha vitendo yaliyo maneno.

Amewashkuru pia wanachama

 Katika maneno yake kwa kuwashkuru wanachama cha RPF amesema

“tunajua matokeo ya uchaguzi ikiwa kuna yeyote anayeumia ajiumize mwenyewe acheni shughuli  za uchaguzi ziwe za furaha. Inafaa kufurahia wale tulio kwa namna ile tunavyoifikiria na pale tunapotaka Rwanda kufika yote ni kwa sababu ya historia yetu ya pekee”.

 

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.