kwamamaza 7

Marekani yaomba ushirikiano nchi zikiwemo Rwanda ili kupambana na ISIS nchini DR Congo

0

Balozi wa Marekani nchini DR Congo Mike Hammer ameomba ushirkiano nchi mbali mbali zikiwemo Rwanda kwa kupambana na kundi la kigaidi, Islamic State nchini humo.

Balozi Hammer ametangazia Radio Okapi kwamba anakusanya habari husika kuhakikisha kama ISIS ingali nchini DR Congo.

“ Tunafanya upelelezi kujua walivyotangaza Daeshi [ISIS]. Lakini kundi kama hili linapotuma ujumbe kama ule, inamaanisha kitu fulani.” Balozi Hammer amesema

“ Haina budi kujua ushirikiano kati ya ADF na Daesh. Ni murua kuomba ushirikiano wa kimataifa kupambana na hili kundi la kigaidi.”

Hata hivyo, Hammer amekubali ISIS ina mpango wa kuwa imara nchini DR Congo.

Amesema kunahitajika ushirikiano wa nchi zikiwemo Burundi na Uganda.

Wiki iliyopita, ISIS ilijigamba mashambulizi nchini DR Congo na ushirikiano wake na wanamgambo wa ADF.

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.