HABARI MPYA

Marekani kupiga marufuku bidhaa kutoka  Rwanda kwenye soko lake

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa nchi yake itapiga marufuku bidhaa kutoka Rwanda kwenye soko lake miezi miwili ijayo.

Rais Trump kupitia barua aliyowandikia mabunge na maseneta wa Marekani ameeleza kwamba Rwanda itakoma kushiriki katika mkataba wa AGOA (American Growth and Opportunity Act) ambao unazirahisishia nchi za nchini ya jangwa la Sahara kuuza baadhi ya bidhaa zake bila kodi nchini Marekani.

Huyu kiongozi amesema kuwa Rwanda inaendelea kuwa kipingamizi cha baadhi ya bidhaa kutoka marekani kama vile kafa ulaya maarufu kama ‘Mitumba’ bila kujali jitihada za marekani kutatua hili suala.

Barua ambayo Sauti ya Marekani imeitupia jicho inaeleza kwamba Rais Trump anaiona Rwanda haina nia ya kuondoa  vipipingamizi vya sela za kiuchumi na uwekezaji wa Marekani kulinagana na makala 104 ya mkataba wa AGOA.

Hata hivyo, Rais Trump amesema kwamba uamuzi huu wa  kutoifukuza Rwanda katika mkataba wa AGOA  ni kuonyesha jitihada za Rwanda na Marekani kulitatua hili suala.

Pia,Trump amesisitiza kuwa ataendelea kuchunguza kama serikali ya Rwanda itapiga hatua yoyote kuondoa vipingamizi kwa kutii   mkataba wa AGOA na kuwa huu uamuzi utaisukuma kurekebisha uamuzi wake

Kwa upande wa Rwanda, Rais wake Paul Kagame kabla ya kuwania urais mwaka 2017 alisema kwamba Rwanda itaendelea kupiga marufuku kafa ulaya hata kama Marekani ilitangaza kuboresha mkataba wa AGOA kwa nchi za Tanzania,Uganda na Rwanda

Pia Kagame aliongeza kuwa hizi nchi zitaanzisha viwanda vyake.

Subscribe to BWIZA TV to get news and song updates

click here to receive the updated news on facebook on twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top