Majina ya watu watano ambayo yanasikika kama ya Wanyarwanda yamejitokeza kwenye orodha ya watu ‘walioshiriki’ katika mambo ya ‘kusajili’ Wanyarwanda 43, ambao walikamatwa wakijaribu kuvuka mpaka kati ya Tanzania na Uganda,Kikagati kwa kutumia hati zinasomekana kuwa ‘bandia’.
Taarifa za chombo cha habari nchini Uganda Virunga post zimeeleza kwamba bilashaka walioshiriki katika kitendo hiki ni Dk.Ruvumwa aliyewahi kutekwa nyara kisha akaachiwa huru,Geoffrey Musoni ambaye aliwahi kuwa mwanajeshi wa Rwanda(RDF),ambaye ni mkazi wilayani Mukono,Moses Bijura ambaye ni mkazi wilayani Ntungamo,Charles Sande maarufu kama Robert Mugisha na mwingine kwa jina la Felix Mwizerwa.
Taarifa hizi zinaendelea kusema kwamba hawa wanaendelea kusajili watu wengine wa kujiunga na jeshi la RNC nchini DR Congo eneo la Minembwe kwa msaada wa maafisa wa upelelezi wa Uganda,CMI.
Pamoja na haya,lengo la safari ya Wanyarwanda hawa lilizusha mkanganyiko kwa kuwa baadhi ya vyombo vya habari vilisema kwamba hawa walikuwa wakielekea nchini Burundi katika shughuli za kidini taarifa ambazo ni tofauti ni nyingine zilizoenea kwamba hawa walikuwa wamesajiliwa kujiunga na jeshi la RNC la jenerali Kayumba Faustin Nyamwasa ‘linalodhamiria’ kuishambulia Rwanda.
Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter
Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com