kwamamaza 7

Majenerali wa jeshi la Rwanda watatu wastaafu pamoja na wanajeshi wengi.

0

Kwenye hatua yake ya 2017 ya kuwastaafu mafisa jumla ya majeshi 817 ndio waliostafu ikiwa ni mara ya tano tangu 2013. Maafisa hawa ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria maalum ya RDF ni pamoja na maofisa 369 na 378 ambao kandarasi yao imefikia mwisho na wengine 70 ambao wamestaafu kwa sababu ya misingi ya afya.

Miongoni mwa majeshi waliostaafu wamo majenerali watatu ambao ni Lt.Gen.Karenzi Karake, Maj Gen Jack Nziza na Brig. Gen. John Gashayija Bagirigomwa.

Waziri wa usalama,Gen James Kabarebe ambaye amekuwa mheshimiwa mkuu katika hafla hii amesema “kwa niaba ya Kamanda mkuu wa jeshi, ningependa kuwapa shukrani za dhati na kuridhika kwa wale ambao wanastaafuu siku ya leo kwa kujitolea kwao katika vita vya kuikomboa nchi na hata kwa mchango wanaoendelea kutoa kwa maaendeleo ya nchi”

Aliongeza pia kwamba ustadi wao na uzoefu ungali unatakiwa kwa maendeleo ya nchi na wakati wowote watakapotakiwa.
Majenerali hao waliostaafu walikuwa na nyadhifa mbalimbali ambako Lt Gen Karenzi Karake amekuwa mshauri wa mambo ya usalama kwenye ikulu, Maj Gen Jack Nziza amekuwa Mkuu wa idara ya J-9 kwenye wizara ya Usalama na Gashayija ambaye amekuwa Kamanda wa idara ya majeshi la akiba kwenye Jimbo la Kaskazini.

Lt Col Rene Ngendahimana ambaye amekuwa msemaji wa Jeshi la Rwanda na hata mshauri wa sheria wa muda naye ni miongoni mwa waliostaafu.
Uadhifa wa Usemaji wa jeshi la Rwanda umechukuliwa na Brig Gen Ferdinand Safari.

Lt Gen Karenzi Karake ambaye amehotubia kwa niaba ya wastaafu amemshukuru Kamanda Mkuu wa jeshi la Rwanda ambaye ni Mh.Paul Kagame kwa ushauri wake na maadili kwenye kazi yao ya kijeshi.

Richard Wa Billy

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.