kwamamaza 7

Mahakama yapiga marufuku rufaa ya aliyewahi kuwa mlinzi wa Rais Kagame

0

Mahakama ya Rufaa nchini Rwanda imepiga marufuku ombi la aliyewahi kuwa mmoja mwa walinzi wa Rais Kagame, Luteni Joel Mutabazi la kuachiwa huru.

Mutabazi aliambia mahakama kwamba anahitaji kuachia huru ili kutibiwa ugonjwa wa macho, Hepatitis na presha.

Jaji tarehe 21 Juni 2019, alisema maelezo yake Luteni Mutabazi hayastahili aachiwe kwa kuwa anakubali kwamba anakutana na waganga wanaomtibu.

Maelezo yake mengine kama vile kufungwa vibaya na kupatiwa chakula kisichohusiana na uzito wa ugonjwa wake pia yamepigwa marufuku.

Luteni Mutabazi anashtakiwa vitendo vya kigaidi, mauaji, kuhatarisha usalama wa nchi . Hata hivyo, analaani mashtaka yote.

Kesi hii itaendelea tarehe 25 Juni 2019.

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.