kwamamaza 7

Mahakama ya kutetea haki za binadamu barani Afrika kuadhibu uhalifu wa kubadili katiba

0

Mahakama ya kutetea haki za binadamu barani Afrika imetangaza kuwa miaka kumi ijayo itaanza kuadhibu uhalifu wa kubadili katiba mala nyingine unaofanywa na marais  barani Afrika.

Mhenga wa mambo ya sheria wa mahakama hii,Me Ibrahima Kane amesema kuwa kubadilisha katiba kinyume na sheria kwa marais waliochaguliwa ama wanaopindua serikali ni ukiukaji wa haki za binadamu na kuwa wanatafuta fursa barani Afrika ya kuhukumu uhalifu huu.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Watakaofanya uhalifu huu waweza kujikuta wakihukumiwa na mahakama hii”Me Ibrahima amenena.

Me Ibrahima ameongeza kuwa kuna uhalifu mpya utakaohukumiwa kama vile utekanyara wa mashua huko nchini Somalia na pengine,ruswa ya hali ya juu,uchuuzi marufuku wa silaha na wanamgambo na mengine.

Akijibu swali la mtangazaji wa VOA kuhusu ewezekanaji wa jambo hili,Me Ibrahima amesema kuwa vinawezekana sana kwa kutoa mfano wa Rwanda,kulikohukumiwa washiriki wa mauaji ya kimbali na nchini Sierra Leone.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mkurugenzi wa mahakama hii,jaji Sylivain Ore ameleza kuwa haitakuwa rais kutia kivitendo hukumu zake kwa kuwa zitakuwa zinahusiana na marais wan chi za Afrika.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Mahakama hii imetangaza  hili wakati ambapo idadi ya marais barani Afrika wanaobadili katiba wanaongezeka jambo linalozusha ghasia katika nchi kadhaa kama vile DR Congo,Uganda,Burundi na pengine.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

 

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.