kwamamaza 7

Maafisa Wakuu wa Polisi wa Rwanda na Tanzania wajadili usalama wa mipaka

0

Maafisa wakuu wa Polisi ya Rwanda na Tanzania wamekuwa wakijadili usalama wa mipaka ya nchi hizo mbili baada ya Simon N. Sirro Kiongozi Mkuu wa Polisi ya Tanzania kutua Rwanda kwa ajii ya ziara ya siku nne.

Simon Sirro alipokewa na mwenzake IGP Emmanuel K.Gasana Afisa Mkuu wa Polisi ya Rwanda  kwenye makao makuu ya Polisi yaliyoko Kacyiru.

Mkutano wao ambao unafanyika kwa mara ya tatu unahusu mkataba wa ushirikiano uliopigiwa sahihi mwaka wa 2012 na wakuu wan chi hizo ambao unalenga kupambana na uhalifu wa kuvuka mpaka na uhusikaji wa wananchi wa nchi hizo mbili katika uhalifu, ikiwemo kusafirishwa kwa madawa ya kulevya, kujikinga na kudhibiti majanga na kuhakikisha usalama unadumishwa katika ushoroba wa kati.

IGP Gasana alisema wakuu wa nchi hizo mbili walitoa mwangaza wa namna ya kushirikiana na kusaidiana.

“kinachobaki kwa sasa na kazi inayotukabili ni kushughulikia kwa mara ushirikiano wetu kwenye safari ya kulinda usalama” amesema IGP Gasana.

[xyz-ihs snippet=”google”]

Ameorodhesha mambo muhimu ambayo yatatiliwa mkazo baina ya nchi hizo mbili ambayo ni pamoja na kujijengea uwezo, kupitia mafunzo, kupashana utendaji mzuri na wahalifu, kutia mkazo maendeleo ya teknolojia na kuchukuwa hatua madhubuti za kupambana usafirishwaji wa madawa ya kulevya.

“Jitihada ya kudumisha usalama wa ardhi ya nchi zetu unakwenda moja kwa moja na maendeleo. Tunahitaji kuimarisha ushirikiano wetu kwa kurahisisha maendeleo ya wananchi wetu na maisha bora yao” amesema.

Simon Sirro amesema ongezeko la mapato na bidhaa zinazopelekwa nje kati ya nchi hizo mbili zitategemea usalama, na ambao huvutia wawekezaji na hata kurahisisha maendeleo.

“tumejumuika hapa kwa nia moja, usalama wa wananchi wetu. Kutembea bila kizuizi kwao, mawazo kuhusu mitaji na biashara yameongezaka na kuwa pana, hivyo kuwaletea wananchi manufaa kadhaa” amesema IGP Sirro.

Sirro alipata fursa ya kuzizuru idara mbalimbali za polisi ya Rwanda ikiwemo Isange One Stop Center – ambayo inawapa huduma za bure za kimatibabu, kisheria waathirika unyanyasaji wa kijinsia na wa watoto , alizuru pia Chuo cha Mafunzo ya Askari Polisi cha Gishari.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Richard Wa Billy

 

Leave A Reply

Your email address will not be published.

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.