HABARI MPYA

Kutoelewana kati ya Rwanda na Uganda kwaweza kukumba mawasiliano na miradi ya maziwa makuu

Kwa mjibu wa taarifa za The East African,kutoelewana kati ya Rwanda na Uganda vita  kunaweza kuharibu mno mawasiliano na miradi mbalimbali  kati ya nchi hizi na kwa eneo la maziwa makuu kwa ujumla.

Taarifa hizi zinasema kuwa kutoelewana kumeanza kuathiri mawasiliano ya nchi hizi jirani na kuwa kunasemekana kuwa mafisa wa Uganda wameanza kuwa tahadhari ya Wanyarwanda wanaovuka boda kuelekea nchini Uganda.

n

Wangaalizi wanasema kuwa jambo hili likiendelea vile vile litaharibu mno  ushirikiano wa Afrika Mashariki kama vile miradi ya miundo mbinu ya ukanda wakati.

Pia kuna taarifa madhubuti zilizoifikia The East African kwamba kila upande husika umeisha toa maonyo kwa wakazi wake kuwa makini wakati wa kutembea ama kufanya shughuli za kila siku.

Akizungumza kuhusu hili,katibu hali kwa mambo ya Muungano wa Afrika Mashariki wa Rwanda,Olivier Nduhungirehe amesema kuwa suala hili linatatuliwa vilivyo kupitia namna sahihi.

Ikiwa tunayoyaona katika vyombo vya habari ni ukweli,kutakuwepo madhara ila si kwa ushirikiano kati ya Rwanda na Uganda tu,ni kwa EAC kwa ujumla”ameleza Dkt.Christopher Kayumba,mwalimu mkuu chuoni na mchambuzi wa mambo ya siasa.

Mwalimu huyu ameongeza kuwa madhara ya mambo sawa na haya ni kuathiri mawasiliano kati ya watu,shughuli za biashara na kuharibu miradi ya ushirikiano wa eneo.

Pamoja na haya,kunasemekana vita baridi kati ya Rwanda na Uganda juu ya na upelelezi,kuwakamata na kuwatesa wakimbizi na kutotimiza miradi mbalimbali.

Bonyeza hapa kupata habari za hivi karibuni kwenye facebook na twitter

Fred Masengesho Rugira/Bwiza.com

Maombe
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Most Popular

To Top